• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Serikali |
    • Malalamiko |
Siha District Council
Siha District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serekali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Siha

  • Mwanzo
  • Historia
    • Dhima na Dira
    • Wasifu wa Wilaya
  • Utawala
    • Muundo wa Kiutawala
    • Idara
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Kilimo,Ushirika na Umwagiliaji
      • Idara ya Mipango,Takwimu na Umwagiliaji
      • Idara ya Elimu Msingi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
    • Kata
      • Sanya Juu
      • Gararagua
      • Karansi
      • Biriri
      • Songu
      • Makiwaru
      • Olkolili
      • Ormelili
      • DonyoMuruak
      • Ngarenairobi
      • Ndumet
      • Mitimirefu
      • Livishi
      • Nasai
      • Kirua
      • Kashashi
      • Ivaeny
  • Huduma zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za maji
    • huduma za Watumishi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Tourism
  • Machapisho
    • Fomu za Maombi
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria
    • Jarida Mtandaoni Kila mwezi
  • Kituo cha habari
    • Maktaba ya Picha
    • Videos
    • Hutuba
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Elimu,Afya na Maji
      • Ujenzi,Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
      • Wajumbe Mkutano wa ALAT
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba vikao 2022/2023
    • Ratiba M/Kiti Halmashauri

Wanawake Siha Wapatiwa Mikopo ya Milioni 36

Posted on: May 29th, 2017


Wanawake Siha wapatiwa Mikopo ya Milioni 36

Halmashauri ya Wilaya ya Siha Mkoa wa Kilimanjaro imetoa kiasi cha shilingi milioni 36 kutoka mapato ya ndani kwa ajili ya kuwainua kiuchumi Wanawake wa Wilaya hiyo.

Mikopo hiyo yenye masharti nafuu imetolewa na Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Aisha Amour katika zoezi la utoaji wa mikopo lililofanyika tarehe 29.5.2017 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Siha.

Kabla ya kutoa mikopo hiyo, katibu Tawala mkoa wa Kilimanjaro ambaye alikuwa mgeni rasmi katika zoezi hilo,aliwataka Wanawake wa Wilaya ya Siha kuitumia mikopo hiyo kwa uangalifu na kwa malengo yaliyopangwa ili kuleta matokeo chanya ndani ya jamii na taifa kwa ujumla.

Aidha,Mhe.Aisha Amour aliagiza Halmashauri zote za Mkoa wa Kilimanjaro kuhakikisha kuwa zinatenga asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa ajili ya mikopo ya Wanawake na Vijana.

Jumla ya vikundi 12 vya Wanawake vyenye wanufaika 249 vilipatiwa mikopo ya Shilingi milioni 3 kwa kila kikundi na viliahidi kutumia fedha hizo kwa malengo yaliyowekwa na kuirejesha mikopo hiyo kwa wakati . Fedha zilizotolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Siha ni sehemu ya asilimia 5 ya Mapato ya ndani ya Halmashauri.

Katika mwaka huu wa fedha 2016/2017 Halmashauri ya Wilaya ya Siha kipindi cha mwezi Agost mwaka 2016 ilitoa Mikopo kwa vikundi 10 vya Wanawake Wilayani Siha vilivyokuwa na wanufaika 157 yenye thamani ya Shilingi milioni 20 ambapo kila kikundi kilipatiwa mkopo wa Shilingi milioni mbili.

Halmashauri ya Wilaya ya Siha ina jumla ya vikundi 532 vya kiuchumi na Ujasiriamali kwa Wanawake na Vijana,Vikundi hivi vinajumla ya Wanufaika wanachama 8730.

Halmashauri ya Wilaya ya Siha katika utekelezaji wa bajeti yake kila mwaka imekuwa ikitenga asilimia 5 ya Mapato ya ndani kwa ajili ya Mikopo ya Wanawake na asilimia 5 kwa ajili ya Vijana.


Baadhi ya Kina mama wa Siha wakisubiri mikopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Siha

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA WALIOITWA KAZINI SIHA DC OKTOBA 2024 October 21, 2024
  • TANGAZO LA KOSEGEZWA MBELE UKODISHAJI WA MASHAMBA January 22, 2025
  • TANGAZO NAFASI YA MWENYEKITI BODI YA AJIRA HALMASHAURI YA SIHA KILIMANJARO February 18, 2025
  • TANGAZO NAFASI ZA KAZI SIHA August 28, 2020
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • MILIONI 316.5 YATOLEWA KWA VIKUNDI 48 WILAYANI SIHA

    May 23, 2025
  • Mchengerwa awapongeza Maofisa Habari Nchini Kwa uchapa kazi

    May 23, 2025
  • Mchengerwa awapongeza Maofisa Habari Nchini Kwa uchapa kazi

    May 23, 2025
  • Mchengerwa awapongeza Maofisa Habari Nchini Kwa uchapa kazi

    May 23, 2025
  • Ona Zote

Video

WATUMISHI SIHA DC WAASWA KUFANYA KAZI KWA UADILIFU
Video zingine

Viunganisho vya haraka

  • Wasifu wa Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Wasifu wa Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri
  • Soma taarifa zote ndani ya tovuti
  • Blog ya Halmashauri
  • facebook ya Halmashauri
  • Matokeo ya Taifa Darasa la Saba 2016 Siha
  • kuomba pasipoti kupitia mtandaoni
  • WARAKA WA MAVAZI KWA WATUMISHI WA UMMA
  • Fomu za Likizo Watumishi wa Umma

Viunganisho Vinavyohusiana

  • Basic Education Statistics
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Takwimu za taifa
  • Idara ya habari maelezo
  • tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Wananchi Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotazama

free HitCounter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji,Halmashauri ya Wilaya ya Siha /Siha District Council

    sanduku la Posta: 5 BR- Sanya Juu -Elerai S.L.P 129, 25482 SIHA

    simu: 0272-970677

    Mobile: 0713164432 DED Siha

    Email: ded@sihadc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani Ya eneo

Copyright ©2017 SihaDistrictCouncil . All rights reserved.