• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Serikali |
    • Malalamiko |
Siha District Council
Siha District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serekali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Siha

  • Mwanzo
  • Historia
    • Dhima na Dira
    • Wasifu wa Wilaya
  • Utawala
    • Muundo wa Kiutawala
    • Idara
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Kilimo,Ushirika na Umwagiliaji
      • Idara ya Mipango,Takwimu na Umwagiliaji
      • Idara ya Elimu Msingi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
    • Kata
      • Sanya Juu
      • Gararagua
      • Karansi
      • Biriri
      • Songu
      • Makiwaru
      • Olkolili
      • Ormelili
      • DonyoMuruak
      • Ngarenairobi
      • Ndumet
      • Mitimirefu
      • Livishi
      • Nasai
      • Kirua
      • Kashashi
      • Ivaeny
  • Huduma zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za maji
    • huduma za Watumishi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Tourism
  • Machapisho
    • Fomu za Maombi
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria
    • Jarida Mtandaoni Kila mwezi
  • Kituo cha habari
    • Maktaba ya Picha
    • Videos
    • Hutuba
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Elimu,Afya na Maji
      • Ujenzi,Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
      • Wajumbe Mkutano wa ALAT
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba vikao 2022/2023
    • Ratiba M/Kiti Halmashauri

Wasifu wa Wilaya

UTANGULIZI

Halmashauri ya Wilaya ya Siha ilianzishwa rasmi tarehe 01.07.2007 kwa sheria No 7 ya mwaka 1982 .na kuwa miongoni mwa Wilaya Sita za Mkoa wa Kilimanjar,Wilaya nyingine ni Rombo,Same,Mwanga,Hai na Moshi. Wilaya ya Siha ina Jimbo moja la uchaguzi, Tarafa 5 nazo ni Siha Magharibi,Siha Kati,Siha Mashariki,Siha Kusini na Siha Kaskazini.Wilaya pia inazo Kata 17,Vijiji 60 na Vitongoji 169.

Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 Wilaya ya Siha inajumla wa watu 139,019 wanaume wakiwa 67,293 na Wanawake wakiwa 71,726.

MIPAKA 

Wilaya ya Siha inakadiriwa kuwa kati ya nyuzi za Longitudi 37.3”-37.17’’ upande wa mashariki na Latitudi 2.5’’ hadi 3.00’’ kusini. Wilaya ya Siha inajumla wa ukubwa wa eneo la kilomita za  mraba 1158 na Wilaya imepakana na Wilaya ya Hai upande wa Kusini,Wilaya ya Longido na Rombo upande Kaskazini Magharibi,Wilaya ya Meru na Hai upande wa Kusini Mashariki.Upande wa Mashariki imepakana na hifadhi ya mlima Kilimanjaro.

Wilaya ya Siha ina Makabila zaidi ya 125 wengi wakiwa ni wachagga,Wamasai na Makabila mengine kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania. Shughuli kubwa za kiuchumi kwa wananchi na wakazi wa Wilaya ya Siha ni kilimo na ufugaji ambapo watu wachache wanajishughulisha na biashara ndogo ndogo na biashara za kati.

UTAWALA

Wilaya ya Siha imeundwa kwa Utawala kuanzia ngazi ya Serikali kuu Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Halmashauri ya Wilaya. Kwa upande wa Halmashauri utawala umepangwa kuanzia Baraza la  Wah.Madiwani,Mkurugenzi Mtendaji,Wakuu wa Divisheni na Vitengo,Maofisa na Watumishi wengine wa Serikali kuanzia ngazi ya Makao Makuu hadi Watumishi waliopo ngazi ya Vijiji na Kata. Halmashauri ya Wilaya ya Siha inajumla ya watumishi wa Umma 1206 wengi wa watumishi hawa wakiwa ni  katika sekta ya Elimu na Afya

SHUGHULI ZA KIUCHUMI

Wananchi na wakazi wengi wanaoishi katika Wilaya ya Siha wanafanya shughuli za Kilimo na Ufugaji katika kuinua kiwango cha uchumi kuanzia ngazi ya Kaya,Kijiji,Kata,hadi Wilaya. Mazao makuu ya chakula yanayolimwa katika Wilaya ya Siha ni pamoja na Maharagwe,Mahindi,Viazi mviringo, Mbaazi,Ndizi na mazao ya mboga mboga. Aidha Mazao ya biashara yanayolimwa katika Wilaya ya Siha ni pamoja na Kahawa,Shairi,Ngano,Parachichi,Karanga Mti na Miti ya Mbao katika shamba la miti West Kilimanjaro.

UWEKEZAJI NA VIVUTIO VYA UTALII

Wilaya ya Siha ni miongoni mwa Wilaya chache katika mkoa wa Kilimanjaro zenye mashamba makubwa na yenye rutuba yaliyopo katika maeneo mazuri yenye kupata mvua za kutosha mara mbili kwa mwaka kutoka kilele cha mlima Kilimanjaro na Mlima Meru. Mashamba haya yamekuwa chanzo kikubwa cha kuendeleza kilimo cha mazao ya biashara na yale ya chakula yanayosafirishwa nje ya Wilaya ya Siha na kusaidia kuongeza mapato ya ndani ya Halmashauri kupitia utozaji wa ushuru wa mazao hayo.

Aidha, Watalii wengi wanaopanda mlima Kilimanjaro kupita lango la Londorosi hadi Shira platu hupitia katika Vijiji na Vitongoji mbalimbali vya Wilaya ya Siha na kujionea tamaduni mbalimbali za Wananchi na wakazi wa Wilaya ya Siha. Wilaya ya Siha  ndiyo Wilaya ya pekee katika mkoa wa Kilimanjaro yenye bustani ya Wanyama pori na kuwa kivutio kikubwa kwa wageni wa ndani na nje ya Tanzania. Miongoni mwa Wanyama Pori waliopo katika Bustani ya Wanyama inajulikana kama Serval Wildlife ni pamoja na Simba,Twiga,Swala na wengine wengi. Pia  Wilaya ya Siha wapo wanyama wengi wanaonekana kandokando ya barabara inayoelekea West Kilimanjaro kupitia lango la Londrosi .Karibu Wilaya ya Siha ujionee mwenyewe maajabu ya wanyama Pori wanaonekana kwa urahisi na kwa karibu.

Pia Wilaya yetu inayo huduma ya Hoteli mbalimbali zilizopo katika maeneo ya kuelekea hifadhi ya mlima Kilimanjaro na ukifika Wilaya ya Siha ndiyo utaweza kufurahia lodge ya kiutamaduni Osiligilai lodge Maasai Lodge iliyopo umbali mfupi kutoka makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Siha. Lodge hii ndiyo lodge pekee hapa kanda ya Kaskazini inayotoa huduma bora ya chakula na malazi katika mazingira ya asili na hivyo kuvutia wageni wengi wa ndani na nje ya Tanzania tena kwa gharama nafuu.  

HUDUMA ZA KIJAMII

a) AFYA 

Wilaya ya Siha inajumla ya Hospital 3,moja hospital ya taifa ya kifua kikuu(Magonjwa Ambukizi),Hospitali ya Charlotte  na hospitali ya Wilaya ya Siha,Vituo vya afya 5, kimoja cha Serikali na vituo 4 vya mashirika ya dini,Zahanati 14 ,9 za Serikali na 6 za mashirika ya Dini na watu binafsi. Hali ya upatikanaji wa huduma za Afya ni  bora kabisa na hivyo kufanya wageni wengi kupenda kufika Wilaya ya Siha pia wananchi na Wakazi wengi wa Wilaya ya Siha  wanapata huduma za afya kwa wakati na kwa umbali mfupi n a maeneo wanayoishi.

b) MAJI 

Hali ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika Wilaya ya Siha hadi mwishoni mwa mwaka  wa fedha 2022/2023 ni zaidi ya  asilimia 86,ambapo wananchi na wakazi wengi wa Wilaya ya Siha hupata maji ya bomba kwa umbali chini ya mita 400. Kwa ujumla Wilaya ya Siha ni miongoni mwa Wilaya chache hapa nchini zinazowapatia wananchi wake huduma ya maji safi na salama tena ya  uhakika katika siku 7 za wiki masaa 24 ndani ya siku 365 za mwaka.

c) ELIMU

Wilaya ya Siha inajumla ya shule 21 za Sekondari,15 za Serikali na 6 za Mashirika ya Dini.Karibu kata zote za Wilaya ya Siha zina shule za sekondari za Wazazi ambapo wanafunzi hutembea umbali chini ya kilomita 4 kufika shule husika.hali ya miundombinu ya shule za sekondari ni ya kuridhisha.

Kwa upande wa elimu msingi,Wilaya ya Siha inajumla ya shule  za Msingi  74 za Serikali ni 61  na za mashirika ya dini na binafsini 13. Kila mwanafunzi wa shule za msingi na sekondari amepatiwa dawati la kukaa akiwa darasani. Hali ya utoaji wa elimu katika Wilaya ya Siha ni ya kuridhisha kwani watoto wote wa shule za msingi na sekondari wanapata chakula cha mchana wakiwa mashuleni

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA WALIOITWA KAZINI SIHA DC OKTOBA 2024 October 21, 2024
  • TANGAZO LA KOSEGEZWA MBELE UKODISHAJI WA MASHAMBA January 22, 2025
  • TANGAZO NAFASI YA MWENYEKITI BODI YA AJIRA HALMASHAURI YA SIHA KILIMANJARO February 18, 2025
  • TANGAZO NAFASI ZA KAZI SIHA August 28, 2020
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • Rais Samia aendelea kuitangaza Tanzania Kimataifa

    April 11, 2025
  • Rais Samia aendelea kuitangaza Tanzania Kimataifa

    April 11, 2025
  • Uzinduzi Sera ya Ardhi Siha yashiriki

    March 17, 2025
  • Umoja wa Ulaya kuendelea kushirikiana na Tanzania

    March 12, 2025
  • Ona Zote

Video

WATUMISHI SIHA DC WAASWA KUFANYA KAZI KWA UADILIFU
Video zingine

Viunganisho vya haraka

  • Wasifu wa Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Wasifu wa Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri
  • Soma taarifa zote ndani ya tovuti
  • Blog ya Halmashauri
  • facebook ya Halmashauri
  • Matokeo ya Taifa Darasa la Saba 2016 Siha
  • kuomba pasipoti kupitia mtandaoni
  • WARAKA WA MAVAZI KWA WATUMISHI WA UMMA
  • Fomu za Likizo Watumishi wa Umma

Viunganisho Vinavyohusiana

  • Basic Education Statistics
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Takwimu za taifa
  • Idara ya habari maelezo
  • tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Wananchi Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotazama

free HitCounter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji,Halmashauri ya Wilaya ya Siha /Siha District Council

    sanduku la Posta: 5 BR- Sanya Juu -Elerai S.L.P 129, 25482 SIHA

    simu: 0272-970677

    Mobile: 0713164432 DED Siha

    Email: ded@sihadc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani Ya eneo

Copyright ©2017 SihaDistrictCouncil . All rights reserved.