• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Serikali |
    • Malalamiko |
Siha District Council
Siha District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serekali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Siha

  • Mwanzo
  • Historia
    • Dhima na Dira
    • Wasifu wa Wilaya
  • Utawala
    • Muundo wa Kiutawala
    • Idara
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Kilimo,Ushirika na Umwagiliaji
      • Idara ya Mipango,Takwimu na Umwagiliaji
      • Idara ya Elimu Msingi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
    • Kata
      • Sanya Juu
      • Gararagua
      • Karansi
      • Biriri
      • Songu
      • Makiwaru
      • Olkolili
      • Ormelili
      • DonyoMuruak
      • Ngarenairobi
      • Ndumet
      • Mitimirefu
      • Livishi
      • Nasai
      • Kirua
      • Kashashi
      • Ivaeny
  • Huduma zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za maji
    • huduma za Watumishi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Tourism
  • Machapisho
    • Fomu za Maombi
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria
    • Jarida Mtandaoni Kila mwezi
  • Kituo cha habari
    • Maktaba ya Picha
    • Videos
    • Hutuba
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Elimu,Afya na Maji
      • Ujenzi,Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
      • Wajumbe Mkutano wa ALAT
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba vikao 2022/2023
    • Ratiba M/Kiti Halmashauri

Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii


IDARA YA MAENDELEO YA JAMII NA USTAWI WA JAMII  WILAYA SIHA

UTANGULIZI

Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii ni kati ya Idara 13 ambazo zinatekeleza na kutimiza malengo ya Halmashauri ya wilaya ya Siha kwa kuzingatia miongozo ya serikali, Sera na mikakati iliyowekwa.Idara ina mipango ya muda mfupi na muda mrefu ambayo inalenga kuendeleza nakuboresha maisha ya watu katika wilaya ya Siha. Idara ina vitengo ambavyo ni:-

Mipango na Utafiti, Jinsia na Watoto, UKIMWI, TASAF na Uwezeshaji wananchiki-uchumi. Idara ina watumishi wa fani ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii ngazi ya wilaya na Kata ambao wanatekeleza, kusimamia, kufuatilia na kutathimini utekelezaji wa malengo hayo kwa kuzingatia malengo ya Milenia, MKUKUTA na Dira ya Mendeleo ya Taifa ya mwaka 2025.

Maadili ya Msingi ya Idara ni haya yafuatayo:-

  • Kujitoa
  • Uadilifu na Uwajibikaji
  • Timu ya kazi
  • Haki
  • Uwazi
  • Heshima
  • Ufanisi
  • Shirikishi ya usimamizi kuendelea
  • Kujifunza.

Kwa kuzingatia misingi hiyo idara inahamasisha , inaelimisha na kuwezesha Jamii kuwa na Ari ya kutamani maendeleo zaidi ki-uchumi na kijamii kwa kuziwezesha kutambua uwezo walionao wa kubaini matatizo na uwezo wao wa kutumia rasilimali zilizopo kujipatia na kujiongezea kipato cha kujiletea maisha bora zaidi kwa kushirikisha serikali, Mashirika na Taasisi mbalimbali kusaidia jitihada za Jamii katika kujiletea maendeleo yao.

 Idara inatekeleza kazi zake kwa kutathimini vigezo vya maendeleo ya Jamii ya Siha kwa kuangalia:-

  • Mabadiliko ya fikra, Mitazamo ya Utamadunina Mila za Jamii ya Siha.
  • Ongezeko la huduma za Jamii kama vile:- Nyumba bora, Afya, Elimu, Lishe bora, Mazingira Safi na salama.
  • Ongezeko la mapato ya kuwezesha Jamii kukidhi mahitaji ya familia na kuweka akiba ya kujiongezea rasilimali.
  • Kupungua kwa vifo vya watoto na wanawake katika uzazi.
  • Mahitaji ya teknolojia za kisasa.
  • Matumizi na hifadhi ya mazingira.

Kwa kuzingatia vigezo hivi idara imekusudia kupunguza na baadaye kuondoa kabisa umaskini katika Jamii ya Siha na taifa letu kwa jumla.

SHABAHA ZA IDARA :-

  • Haki za watoto kuimarishwa katika vijiji 60 kufikia mwaka 2025.
  • Mikakati:-
  • Kutambua watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi katika vijiji 60 na kuunda kamati za kushughulikia watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.
  • Kutoa mafunzo ya kisaikolojia kwa watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi (MVC) na kamati zinazoshughulikia watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi katika vijiji 60.
  • Kutoa msaada was sare kwa watoto wa shule za msingi na sekondari wanaoishi mazingira hatarishi.
  • Kuhamasisha na kuelimisha Jamii madhara ya mila potofu dhidi ya watoto wa kike, unyanyasaji na ndoa za utotoni katika vijiji 60.
  • Kuunda mabaraza ya watoto katika ngazi ya kata na wilaya.
  • Vikundi vya kijamii na ki-uchumi kuanzishwa na kuimarishwa ifikapo mwaka 2025:-
  • Mikakati:-
  • Kuhamasisha Jamii kuunda na kusajili vikundi vya ki -uchumi na Kijamii katika vijiji 60  kwa ajili ya kujiongezea kipato na kupunguza umaskini.
  • Kutoa elimu na ujuzi wa Ujasiriamali wa vikundi vya ki – uchumi na kijamii
  • Kuwezesha na kutoa mikopo kwa vikundi vya ki – uchumi na kijamii.
  • Kupungua kwa maambukizi ya VVU/UKIMWI kutoka 2.5% hadi 2.0% ifikapo mwaka 2025
  • Kuhamasisha Jamii juu ya upimaji wa VVU/UKIMWI kwa hiyari
  • Kuhamasisha waathirika wa VVU/UKIMWI kujitangaza wenyewe kwa hiyari na kuunda vikundi vya mtandao wao na kuwasaidia.
  • Kutoa elimu ya VVU/UKIMWI kwa kamati za vijiji za kupambana na maambukizi ya UKIMWI ngazi Kata na Vijiji
  • Kufanya maadhimisho ya siku ya UKIMWI kila mwaka
  • Masuala ya Jinsia katika Kata 17 kuimarishwa ifikapo mwaka 2025
  • Mikakati:-
  • Kuhamasisha wanawake kugombea nafasi za Uongozi
  • Kujengea Jamii uelewa kuhusu masuala ya Jinsia
  • Kufanya maadhimisho ya siku ya wanawake kila mwaka
  • Mashirika yasiyo ya kiserikali kuimarishwa ifikapo mwaka 2025
  • Mikakati:-
  • Kutambua mashirika yasiyo ya kiserikali na maeneo yao ya kazi
  • Kuanzisha mitandao ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali
  • Kufanya tathmini utendaji kazi vikao vya Mashirika yasiyo yakiserikali ndani ya Wilaya
  • Uhamasishaji wa Jamii katika vijiji 60 ili kuunda vikundi vya Kijamii (CBO) kwa lengo la kufanya shughuli ndogondogo za kiuchumi
  • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii kuimarishwa ifikapo mwaka 2025
  • Mkakati:-
  • Kuajiri watumishi katika ngazi ya Kata na Wilaya
  • Kuwezesha watumishi wa idara kuhudhuria kozi muda mfupi na za muda mrefu
  • Kuhakikisha upatikanaji wa vitendea kazi katika idara
  • Ushiriki wa watu wenye ulemavu kuimarishwa katika vijiji 60 ifikapo mwaka 2025
  • Mikakati:-
  • Kutambua watu wenye ulemavu na kuchambua mahitaji yao
  • Kuunda na kusajili mtandao wa watu wenye ulemavu
  • Kuwezesha mafunzo ya ujasiriamali kwa walemavu
  • Matumizi ya Teknolojia sahihi na rahisi kuimarishwa katika vijiji 60 ifikapo mwaka 2025
  • Mikakati:-
  • Kujenga uelewa kwa Jamii kuhudu matumizi ya teknolojia sahihi na rahisi katika vijiji 60
  • Kuhamasisha Jamii kuhusu kuhifadhi na utunzaji wa mazingira
  • Kujengea uwezo Jamii kwa kuwaelimisha umuhimu wa matumizi ya teknolojia Sahihi na Nyepesi
  • Haki za Wazee kuimarishwa ifikapo mwaka 2025
  • Mikakati:-
  • Kutambua Wazee wenye umri wa miaka 60 na kuendelea katika vijiji 60
  • Kuhamasisha Wazee kuanzisha na kusajili vikundi vya ujasiriamali katika vijiji 60
  • Kuwashirikisha Wazee katika vikao na mikutano ya maamuzi katika ngazi ya wilaya, Kata na Vijiji
  • Kuwezesha Wazee kupata vitambulisho vya bima ya Afya
  • Uelewa wa Utawala bora kwa viongozi kuimarishwa katika vijiji 60 ifikapo mwaka 2025:-
  • Mkakati:-
  • Kuhamasisha, kuelimisha mabaraza ya kata na serikali za vijiji kuhusu dhana ya utawala bora na utekelezaji wake katika maendeleo endelevu ya Jamii ya Siha.

 11.0    Kupunguza umaskini katika Kaya za Jamii ifikapo 2025

  • Mikakati:-
  • Kutambua Kaya maskini katika vijiji 60
  • Kuunda Kamati za kusimamia na kuratibu Kaya maskini katika vijiji
  • Kuhaulisha fedha za kuwajengea uwezo kiuchumi na kijamii.
  • Kutoa mafunzo ya utawala bora kwa viongozi .
  • Kuwezesha Jamii kwa kufanya kazi kwa bidii, maarifa, nidhamu ili wawe na kipato cha kuwawezesha kuwa na maisha bora na kujitegemea kwa kutumia rasilimali walizonazo.

MAFANIKIO:

Idara ya maendeleo ya Jamii imepata mafanikio tangu Wilaya ya Siha kuanzishwa mwaka 2005 hadi sasa Idara imeendelea kuwa mstari wa mbele katika kuwezesha utekelezaji wa Sera, program, mikakati na kampeni za sekta mbalimbali kutokana na matumizi bora ya mbinu sh8irikishi Jamii kwa kuwezesha Jamii kushiriki katika kufanya maamuzi, kuhusu kupanga, kutekeleza, kufuatilia a kutathimini mipango ya masuala yanayohusu maendeleo yao, kiuchumi, kijamii, kisiasa na kiutawala.

  • Watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi 4144 wametambuliwa na kuwezeshwa huduma mbalimbali za kijamii na kiuchumi.
  • Kamati za kusimamia na kuratibu watoto wanaoishi mazingira hatarishi zimeundwa ngazi ya vijiji
  • Watoto wa kike na wakiume wote wamepata furs asana ya kusoma
  • Ukeketaji na ndoa za utotoni zimepungua
  • Watoto wanashirikishwa katika maamuzi mbalimbali yanayowahusu
  • Jumla ya vikundi vya kiuchimi na kijamii 730 vimeundwa na kusajiliwa
  • Jumla ya vikundo 110 vimepata mikopo na elimu ya ujasiriamali
  • Sekta ya maendeleo ya Jamii imeziwezesha sekta nyingine katika Halmashauri kuwawezesha wananchi kuongeza ari na nguvu katika kukuza uchumi, kupambana na umaskini na kuendeleza utawala bora
  • CHANGAMOTO ZA UTENDAJI KAZI IDARA YA MAENDELEO YA JAMII:-
  • Uimarishaji wa kikosi cha Ujenzi:
  • Kikosi hiki kina mchango mkubwa kwa wananchi katika jitihada zao za kujijengea nyumba bora na miundombinu nyingine ya Kijamii hususani maeneo ya kijijini. Ipo haja ya kuanzisha na kuimarisha kwa nyenzo na rasilimali za kiufundi ili kukidhi matarajio ya wananchi.
  • Uimarishaji wa Ari ya utendaji kazi wa wataalamu wa maendeleo ya Jamii.
  • Kutokana na mabadiliko  yanayotokea miongoni mwa jamii na duniani kote, wataalam hawa wanahitaji kuimarishwa kitaaluma, kimazingira,kimaslahi,kinyenzo nk ili waweze kukabiliana na mabadiliko ya mahitaji katika jamii.
  • Matumizi ya majumba ya maendeleo :

Kujenga majumba ya maendeleo kwa madhumuni mbalimbali ya kijamii yakiwemo mikutano ya kijamii ya kupashana habari za kijamii,mafunzo kwa wanawake kuhusu lishe,utunzaji wa nyumba,ususi,michezo,burudani,kisomo chenye manufaa na kujiendeleza.

  • Uthaminishaji wa mchango wa Jamii katika shughuli za maendeleo:-
  • Wananchi wamekuwa wakichangia nguvu zao katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kama ujenzi wa shule, Zahanati, barabara, visima vya maji na miudombinu nyingine wakisaidiana na juhudi za serikali. Michango hii haionekani waziwazi katika bajeti na hesabu za serikali hivyo kutokuwa na picha sahihi ya pato la taifa ambalo ndilo kigezo kikuu cha kiwango cha maendeleo ya nchi. Ipo haja ya kuthaminisha mchangowa wananchi katika bajeti za serikali ili kuweza kupata picha ya maendeleo ya nchi yetu.
  • Upatikanaji wa wataalamu wa Maendeleo ya Jamii wa kutosha:-
  • Wataalamu wa Maendeleo ya Jamii ndiyo waandaaji wa watu kwa ajili ya kuwawezesha kushiriki Maendeleo yao. Ili waweze kutimiza azma hiyo kunahitajika walao mtaalamu mmoja kila kata.
  • Upatikanaji wa nyenzo na Vitendea kazi vya kutosha:-
  • _ Msingi wa maendeleo ya Jamii unalenga katika kuwezesha watu, kujihudumia katika kujiletea maendeleo endelevu. Ili kutekeleza azma hii wataalamu wa maendeleo ya Jamii wanahitaji kuwezeshwa kinyenzo na vitendea kazi ikiwa ni pamoja na vyombo vya usafiri.
  • Kuwepo kwa mabadiliko chanya ya Tabia za watu:-
  • Jamii inahitaji kuwa na mabadiliko chanya ya kitabia ili kukabiliana na matukio na matatizo yanayojitokeza katika Jamii, kiuchumi, kisiasa na kiutawala. Idara ya maendeleo ya Jamii inaelimisha, inaraghbisha, inahamasisha na kushawishi Jamii kuhusu, manufaa na athari za matukio mbalimbali yanayoonekana katika maisha ya kawaida ya Jamii.
  • Uimarishaji wa vita dhidi ya Ujinga, Maradhi na Umaskini:-
  • Ujinga, Maradhi na Umaskini vinaendelea kuwa maadui wa Maendeleo ya wananchi wa Tanzania tangu tupate Uhuru. Pamoja na serikali kutilia mkazo vita dhidi ya maadui hao, hali ya maisha ya wananchi walio wengi imeendelea kukabiliwa na umaskini wa kipato na magonjwa ya mlipuko. Wataalamu wa maendeleo ya Jamii wanapaswa kuimarisha utoaji wa elimu kwa Jamii kuhusu usafi wa mazingira na kinga dhidi ya maradhi,mbinu bora za kuandaa miradi ya kiuchumi kupambana na umaskini wa kipato.

  

MIRADI MBALIMBALI ILIYOTEKELEZWA NA JAMII KWA LENGO LA KUJITEGEMEA KWA DHANA YA KUSHIRIKI NA USHIRIKISHWAJI

            

Mradi wa ujenzi wa vyumba viwili  vya Madarasa Suumu sekondari kipindi cha 2009/10  (TASAF).

Kiasi cha fedha zilizopokelewa kwa ajili  ya  utekelezaji ni Tsh.19,425,142.50

Jengo hili lipo katika hatua ya umaliziaji sawa na 85% ya ujenzi

Mradi wa jamii wa ujenzi wa vyumba viwili  vya Madarasa Kishisha sekondari kipindi cha 2009/10  (TASAF).

  • Kiasi cha fedha zilizopokelewa kwa ajili  ya  utekelezaji ni Tsh.19,425,142.50

Jengo hili lipo katika hatua ya kupaua sawa na 60% ya utekelezaji

Mradi wa jamii wa ujenzi wa vyumba viwili  vya Madarasa Sanya Juu sekondari  kipindi cha 2009/10  (TASAF).

Kiasi cha fedha zilizopokelewa kwa ajili ya utekelezaji ni Tsh.19,425,142.50

Jengo hili lipo katika hatua ya kufungwa lenta sawa na 55% ya ujenzi

Mradi wa jamii wa ujenzi wa vyumba viwili  vya Madarasa Dahani sekondari kipindi cha 2009/10  (TASAF).

  • Kiasi cha fedha zilizopokelewa kwa ajili ya utekelezaji ni Tsh.19,425,142.50
  • Jengo hili lipo katika hatua ya Msingi kama picha inavyoonesha sawa na 25% ya ujenzi

Mradi wa jamii wa ujenzi wa vyumba viwili  vya Madarasa Dahani sekondari kipindi cha 2009/10  (TASAF).

  • Kiasi cha fedha zilizopokelewa kwa ajili ya utekelezaji ni Tsh.19,425,142.50

Jengo hili lipo katika hatua ya Msingi kama picha inavyoonesha sawa na 25% ya ujenzi

Mradi wa jamii wa ufugaji Mbuzi wa maziwa kwa ajili ya kundi maalum la wazee katika Kijiji cha Samaki maini kipindi cha 2009/10.Jumla ya Mbuzi 41 wamegawanywa(madume 2 na majike 39).Idadi ya walengwa walionufaika na mradi huo ni wazee 39.

Katika picha hiyo anaonekana mzee Vehaeli Mmari ambaye ni moja kati ya wazee walionufaika na mradi huo.Mradi umekamilika kwa 100%

Kiasi cha fedha zilizopokelewa kwa ajili ya utekelezaji ni Tsh 9,733,157.50

Mradi wa jamii wa ufugaji wa Kuku wa mayai kwa ajili ya kundi maalum la waathirika wa VVU/UKIMWI katika Kijiji cha Lawate kipindi cha 2009/10.Jumla ya kuku 200 waligawanywa kwa walengwa10,Ambapo kila mmoja alipewa kuku 20.Hapo ni nyumbani kwa Ndg.Amina J.Mhando.Mradi umekamilikakwa 100%

Kiasi cha fedha zilizopokelewa kwa ajili ya utekelezaji ni Tsh.4,700,523.50

Mradi wa jamii wa ufugaji Mbuzi wa maziwa kwa ajili ya kundi maalum la watoto yatima katika Kijiji chaOlkolili Kipindi cha 2009/10.

Katika picha hii linaonekana banda ambalo limekamilika,na zoezi la kutafuta Mbuzi wanaoweza kumudu mazingira ya eneo husika aina ya Toggenbarg linaendelea.Jumla ya watoto 10 watanufaika na mradi huo,ambapo kila mlengwa atapewa Mbuzi mmoja.

Mradi umekamilika kwa 80%

Kiasi cha fedha zilizopokelewa kwa ajili ya utekelezaji ni Tsh.8,032,722.50

Mradi wa jamii wa ufugaji Mbuzi wa maziwa kundi maalum la wazee katika Kijiji cha Kyengia kipindi cha 2009/10

Mradi huo picha yake haionekani kutokana na kwamba utekelezaji bado haujaanza kutokana na sababu zifuatazo:-

- Pesa kwa ajili ya utekelezaji zilichelewa

- Kiasi cha fedha zilizoingia Halmashauri ni Tsh.9,575,610/=

- Taratibu za kufungua akaunti namba zimekamilika

- Taratibu kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa kamati(CMC Training)zinaendelea

Mradi wa jamii wa ujenzi wa vyumba vitatu vya Madarasa katika shule ya sekondari Kilingi kipindi cha 2007/08  (TASAF).

Jengo hili limekamilika kwa 95%

Kiasi cha fedha zilizopokelewa kwa ajili ya utekelezaji ni Tsh.29,550,620.00

Mradi wa jamii wa ujenzi wa vyumba vitatu vya Madarasa katika shule ya sekondari Magadini  kipindi cha 2007/08  (TASAF).

  • Kiasi cha fedha zilizopokelewa kwa ajili ya utekelezaji ni Tsh.29,550,620.00

Umaliziaji(Finishing) katika jengo hilo haujakamilika kama picha inavyoonesha.

Jengo limekamilika kwa 85%

 

Mradi wa jamii wa ujenzi wa vyumba vinne vya Madarasa katika shule ya msingi Roseline kipindi cha 2007/08  (TASAF).

Umaliziaji(Finishing) katika jengo hilo haujakamilika kama picha inavyoonesha.

Jengo limekamilika kwa 85%

Kiasi cha fedha zilizopokelewa kwa ajili ya utekelezaji ni Tsh.36,067,767.00

Jengo hilo linatumika kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa katika shule hiyo.

 

IMEANDALIWA NA IDARA YA MAENDELEO YA JAMII NA USTAWI WA JAMII TAREHE 25/4/2017

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA WALIOITWA KAZINI SIHA DC OKTOBA 2024 October 21, 2024
  • TANGAZO LA KOSEGEZWA MBELE UKODISHAJI WA MASHAMBA January 22, 2025
  • TANGAZO NAFASI YA MWENYEKITI BODI YA AJIRA HALMASHAURI YA SIHA KILIMANJARO February 18, 2025
  • TANGAZO NAFASI ZA KAZI SIHA August 28, 2020
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • Rais Samia aendelea kuitangaza Tanzania Kimataifa

    April 11, 2025
  • Rais Samia aendelea kuitangaza Tanzania Kimataifa

    April 11, 2025
  • Uzinduzi Sera ya Ardhi Siha yashiriki

    March 17, 2025
  • Umoja wa Ulaya kuendelea kushirikiana na Tanzania

    March 12, 2025
  • Ona Zote

Video

WATUMISHI SIHA DC WAASWA KUFANYA KAZI KWA UADILIFU
Video zingine

Viunganisho vya haraka

  • Wasifu wa Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Wasifu wa Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri
  • Soma taarifa zote ndani ya tovuti
  • Blog ya Halmashauri
  • facebook ya Halmashauri
  • Matokeo ya Taifa Darasa la Saba 2016 Siha
  • kuomba pasipoti kupitia mtandaoni
  • WARAKA WA MAVAZI KWA WATUMISHI WA UMMA
  • Fomu za Likizo Watumishi wa Umma

Viunganisho Vinavyohusiana

  • Basic Education Statistics
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Takwimu za taifa
  • Idara ya habari maelezo
  • tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Wananchi Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotazama

free HitCounter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji,Halmashauri ya Wilaya ya Siha /Siha District Council

    sanduku la Posta: 5 BR- Sanya Juu -Elerai S.L.P 129, 25482 SIHA

    simu: 0272-970677

    Mobile: 0713164432 DED Siha

    Email: ded@sihadc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani Ya eneo

Copyright ©2017 SihaDistrictCouncil . All rights reserved.