• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Serikali |
    • Malalamiko |
Siha District Council
Siha District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serekali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Siha

  • Mwanzo
  • Historia
    • Dhima na Dira
    • Wasifu wa Wilaya
  • Utawala
    • Muundo wa Kiutawala
    • Idara
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Kilimo,Ushirika na Umwagiliaji
      • Idara ya Mipango,Takwimu na Umwagiliaji
      • Idara ya Elimu Msingi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
    • Kata
      • Sanya Juu
      • Gararagua
      • Karansi
      • Biriri
      • Songu
      • Makiwaru
      • Olkolili
      • Ormelili
      • DonyoMuruak
      • Ngarenairobi
      • Ndumet
      • Mitimirefu
      • Livishi
      • Nasai
      • Kirua
      • Kashashi
      • Ivaeny
  • Huduma zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za maji
    • huduma za Watumishi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Tourism
  • Machapisho
    • Fomu za Maombi
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria
    • Jarida Mtandaoni Kila mwezi
  • Kituo cha habari
    • Maktaba ya Picha
    • Videos
    • Hutuba
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Elimu,Afya na Maji
      • Ujenzi,Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
      • Wajumbe Mkutano wa ALAT
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba vikao 2022/2023
    • Ratiba M/Kiti Halmashauri

Mifugo na Uvuvi

IDARA YA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI

  • UTANGULIZI:

Idara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi inasimamia shughuli zote zinazohusiana na Mifugo na Uvuvi katika Wilaya ya Siha. Malengo makuu ya usimamizi huo ni yale ya kitaifa ambayo ni kuhakikisha kwamba sekta ya Mifugo na uvuvi inachangia katika pato la watanzania ambao wanategemea shughuli hiyo kwa kuendesha maisha yao na pato la Taifa. Katika kufikia malengo hayo, idara inajishughulisha kuandaa na kutekeleza mipango mbalimbali ya kuinua kipato cha mwananchi kupitia ufugaji wa mifugo mbalimbali na ufugaji wa samaki. Katika ufugaji wa mifugo mbalimbali, idara imejikita katika kuboresha aina ya Ufugaji wa asili uliokuwepo toka enzi na kuwa na ufugaji bora na wenye tija.

HUDUMA ZINAZOTOLEWA:

  • kutoa elimu ya ufugaji kwa wafugaji,
  • kuhamasisha uundaji wa vikundi vya wafugaji.
  • kusimamia sheria mbalimbali za mifugo na madawa
  •  kuzuia kuenea kwa magonjwa ya mifugo kwa kutibu,kuchanja mifugo,kuogesha na kutoa vibali vya kusafirisha mifugo
  •  kutafuta masoko kwa bidhaa zitokanazo na mifugo.
  • Kufanya ukaguzi wa afya ya mifugo na mazao yake.
  • Kuboresha mifugo kwa njia ya Uhamilishaji.
  • Kuandaa bajeti ya miradi na usimamizi wa miradi.
  • Kuandaa taarifa za kila robo za sekta ya mifugo.
  • MGAWANYO KATIKA IDARA
  • Idara ya mifugo imegawanyika katika  sehemu 5 ambazo ni:
  • Uzuiaji wa magonjwa ya mifugo na usimamizi wa sheria
  • Uzalishaji wa mifugo
  • Ukaguzi na uendelezaji  wa mazao yatokanayo na Mifugo
  • Ufugaji wa wanyama wadogo
  • Ufugaji wa samaki
  • UZUIAJI WA MAGONJWA YA MIFUGO NA USIMAMIZI WA SHERIA

Sehemu hii inajishughulisha na kuhakikisha kuwa magonjwa ya mifugo yanagundulika mapema na hayasambai ndani na nje ya Wilaya.

Kazi zinazofanyika ni kufuatilia kwa karibu kuwepo au kutokuwepo kwa magonjwa  na kuchukua hatua za haraka kabla ugonjwa haujaenea. Ufuatiliaji huu unafanyika kwa kuwatumia wataalamu wa ugani katika kata na vijiji na wananchi kutoa taarifa za kuwepo kwa ugonjwa kwa njia ya simu na sisi kufuatilia.

Chanjo kwa Mifugo: Ipo ratiba ya uchanjaji kwa mwaka kwa baadhi ya magonjwa ambayo ni kipaumbele. Magonjwa hayo ni Kimeta, FMD, kichaa cha mbwa na newcaslte kwa kuku. Kwa kushirikiana na wafugaji, idara inaandaa ratiba na kuwasilisha kwa wafugaji kupitia mikutano na kuwataka kuchangia gharama kwa kila mnyama atakayechanjwa. Ingawa imekua na mafanikio makubwa,  imekuwa na changamoto kubwa kutokana na baadhi ya wafugaji kutoonyesha utayari wa kuchangia gharama hivyo kupelekea kuharibu ratiba ya uchanjaji.

UOGESHAJI MIFUGO: Halmashauri ina Majosho 7 na Sprayrace 1 ambayo hutumika  kuogeshaji mifugo kuzuia magonjwa yatokanayo na kupe. Kwa wafugaji wenye mifugo michache hutumia bomba la mgongoni  kunyunyizia mifugo yao. Taratibu za uogeshaji hufanyika kupitia vikundi vya wafugaji ambavyo hupanga utaratibu mzima wa kupata dawa na kuweka kiwango cha kila mfugaji kulipia anapoogesha mifugo yake. Mtaalamu wa mifugo wa kata au kijiji husimamia uogeshaji na kukusanya takwimu za uogeshaji. Hata hivyo swala la kuogesha mifugo kutumia majosho haya limekua na changamoto kubwa kutokana na kutokua na maenea maalum kwa ajili ya malisho.  Maeneo mengi ni mashamba ya watu hivyo kuwafanya wafugaji kuhamisha mifugo kutoka maeneo hayo wakati wa kilimo na majosho hayo kubaki bila kutumika kwa kipindi chote cha kilimo.

 USAFIRISHAJI WA MIFUGO: Magonjwa huweza kusambaa kwa njia ya usafirishaji wa mifugo na mazao yake kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine iwapo hakuna udhibiti. Kabla ya kusafirisha mifugo,wataalam wa mifugo hukagua mifugo inayotaka kusafirishwa na kutoa kibali baada ya kuridhika kuwa wana afya nzuri na hawana magonjwa ya kuweza kuambukiza.  Sheria ya magonjwa ya mifugo no 17 ya mwaka 2003,inakataza kabisa mtu yeyote kusafirisha mifugo kutoka sehemu moja hadi nyingine bila kuwa na kibali.

  • UZALISHAJI WA MIFUGO:

 Ufugaji wenye tija hauna budi kuzingatia uzalishaji ulio bora. Msingi mkuu wa uzalishaji bora ni kuwa na mbegu iliyobora. Kwa muda mrefu wilaya ya siha imekua ikisifika kwa kutoa mitamba bora yenye kuwa na uzalishaji mkubwa. Hii ilitokana na kuwa na mashamba ya mitamba yaliyokua ya serikali ambayo baadae yaliuzwa kwa wawekezaji. Hata hivyo jinsi muda ulivyokwenda, tija katika mifugo ilianza kushuka kwani wawekezaji hawakuweza kuzalisha tena mitamba kwa njia za kisasa na watu binafsi kuzalisha mifugo yao kwa kutumia madume yasiyo na sifa. Baada ya kugundua kushuka kwa uzalishaji hasa wa maziwa, idara iliandaa program ya kutoa elimu kwa wafugaji na kuhamasisha matumizi ya Teknolojia ya uhimilishaji,matumizi ya madume bora naUnunuzi wa mitamba. Kwa kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali, Wataalamu   15 walipelekwa  katika kituo cha uhimilishaji cha NAIC kilichopo Arusha  kupatiwa mafunzo ya uhimilishaji. Kwa mwaka 2016/2017 halmashauri imetenga bajeti kwa ajili ya kufundisha wataalamu 17 wa uhimilishaji na kuwapa vifaa..  Wastani wa uzalishaji wa ng’ombe wa maziwa umeongezeka kutoka lita 5  mwaka 2014 hadi 8 kwa siku mwaka 2016.

VITUO VYA UHIMILISHAJI: Halmashauri ina vituo viwili vya uhimilishaji ambavyo ni Sanyajuu na Kashashi. Kwa sasa vituo hivyo vinakabiliwa na changamoto ya uchakavu wa majengo na vifaa vya uhamilishaji. Vituo hivi pia hutumika kama vituo vya tiba na uchunguzi wa magonjwa ya mifugo. Kwa mwaka 2016/2017, Halmashauri imetenga bajeti kwa ajili ya ukarabati.

  • UKAGUZI NA UENDELEZAJI WA MAZAO YA MIFUGO: Ukaguzi unalenga katika kulinda ubora,afya za walaji wa mazao ya mifugo na  kuzuia kuenea kwa magonjwa ya mifugo.
  • UKAGUZI WA NYAMA: Ni kitendo cha kukagua na kuchunguza mnyama kama anastahili kuchinjwa na kukagua nyama yake baaada ya kuchinjwa ili kurushu nyama hiyo kutumika au kutotumika kama kitowea. Lengo kuu ni kuzuia magonjwa ambayo yapo kwenye mifugo na yanaweza kumuambukiza binadamu anapotumia nyama hiyo, kutambua magonjwa ambayo kwa nje hayakuweza kuonekana ila yapo kwa mnyama ili kuchukua tahadhari kwa wanyama walioko hai.
  • - wanyama wote wanaochinjwa kwa matumizi ya binadamu, ni lazima wakaguliwe na mtaalamu wa mifugo aliyeteuliwa na mahali palipoidhinishwa(Machinjio)
  • -Ni kosa kisheria kuchinja na kuuza nyama yoyote na mahali popote bila kukaguliwa na kupata kibali toka kwa mtaalamu wa Mifugo/mkaguzi
  • - kwa mtu yoyote anayetaka kuchinja mnyama wake kwa ajili ya sherehe,misiba au matumizi binafsi, anawasiliana na mtaalamu wa mifugo wa eneo lake kwa ajili ya kupata huduma ya ukaguzi.

4.0  UKAGUZI WA MAZIWA: Ukaguzi wa maziwa unafanyika katika vituo vya ukusanyaji maziwa. Lengo kuu la ukaguzi ni kutambua ubora wa maziwa yanayouzwa kwa lengo la kulinda walaji na kulinda soko la maziwa.  Maziwa yanaweza  kuchafuliwa kwa makusudi kwa kuongeza maji au bidhaa nyingine kwa lengo la kujipatia faida kubwa kwa muuzaji. Pia maziwa yanaweza kusababisha magonjwa ya kuharisha kwa kutosafisha vyombo vinavyotumika. 

Ukaguzi wa maziwa katika maeneo yetu una changamoto kubwa kutokana na maziwa mengi kuuziwa majumbani kabla hayajapelekwa kwenye vituo. Wananchi wanashauriwa kuchemsha maziwa vizuri kabla ya kutumia ili kuepukamagonjwa kama brucella na TB.

  • UFUGAJI WA WANYAMA WADOGO WADOGO JAMII YA NDEGE: wanyama wadogo a jamii ya ndege hufugwa kwa asilimia zaidi ya tisini na tano ya kaya zilizopo siha. Hii ni kwa sababu ya sifa zao kubwa ambazo ni mahitaji madogo ya eneo, chakula kidogo, mtaji mdogo wa kuanzishia na na gharama kidogo za kuwahudumia. Wanyama hao ni kuku, bata, sungura na kanga. Pamoja na udogo wao,wanyama hawa wana mchango mkubwa sana kwa jamii.
  • UFUGAJI WA SAMAKI: Wilaya ya siha haina mito wala mabwawa ya asili ya uvunaji wa samaki.  Hata hivyo wapo wananchi wachache ambao wanafuga samaki kwenye mabwawa  waliyochimba kwa matumizi ya nyumbani.  Uhamasishaji ufugaji wa Samaki umekua ukifanyika kupitia kwa maafisa ugani na mafanikio yameanza kuonekana kwa watu kuwa na mwitikio chanya. Ufugaji wa samaki hauna gharama kubwa  unapokuwa umechimba bwawa lako. Ni matumaini yetu kuwa watu wengi watahamasika na ufugaji wa samaki kwa siku zijazo.

6.0   AINA YA MIFUGO NA IDADI.

Na
Aina ya mifugo
Idadi
1
Ngombe
56,781
2
Mbuzi
58,824
3
Kondoo
57,230
4
Nguruwe
6,387
5
Kuku
138,543
6
Mbwa
2,963
7
Punda
4,454
JUMLA

NB. Idadi hiyo hapo juu imepatikana kutokana na sense ya ndani iliyofanywa na maafisa ugani wa vijiji na kata kwa kushirikiana na Viongozi wa vijiji novemba 2015

7.0   AINA ZA UFUGAJI

 Kuna aina tatu za ufugaji katika wilaya ya Siha

1. Ufugaji wa ndani ( zero grazing), aina ambayo hutumiwa sana na wafugaji wa mlimani ambao hufuga ng’ombe wa Maziwa. Ngombe hufungiwa kwenye banda na kuletewa majani na maji. Kutokana na utamaduni wa kichaga, Ng’ombe hukaa sehemu ambayo hatakiwi kuonekana na kila mtu anayeingia kwenye kaya hiyo. Wananchi wanaoendesha ufugaji wa aina hii pia hujishughulisha na shughuli za kilimo. Mabaki ya mazao hutumika kwa ajili ya kulishia mifugo. Mabaki haya hukusanywa kwenye maghala na kutumika zaidi wakati wa kiangazi ambapo malisho mengine hayapo.

2. Ufugaji wa Kuchunga (free nange system), aina hii ya ufugaji hutumiwa na wananchi wanaoishi katika maeneo ya tambarare. Wenyeji wa maeneo hayo ni wameru na wamasai ambapo kwa asili ni wafugaji. Hata hivyo nao hujishughulisha na shughuli za kilimo kwa ajili ya kupata mahitaji ya chakula. Wakati wa kilimo, mifugo huhamishwa kwenda maeneo mengine ambayo hayatumiki kwa kilimo na pindi wanapovuna mifugo hurudishwa mashambani kutumia mabaki ya mazao. Kitendo cha wafugaji kujishughulisha na kilimo, kimesaidia kupunguza migogoro ya wafugaji na wakulima kwani kila mtu anaheshimu mali ya mwenzake.

8. WATUMISHI WA MIFUGO:      

Kwa sasa Idara ya Mifugo in wafanyakazi  (30), watatu wapo makao makuu na 27 wapo katika kata na vijiji. Kuna upungufu wa watumishi 33 ili kila kijiji kiwe na mtumishi wa Mifugo. Kazi za Maafisa ugani (Majina mengine; bwanashamba, bibi shamba,bwana mifugo, bibi mifugo,mganga wa mifugo) wa kijiji na kata ni kutoa ushauri wa kitaalam kwa wakulima na wafugaji, kutoa huduma ya kutibu na kufanya uchunguzi wa magonjwa ya mifugo, kufanya ukaguzi wa mifugo, nyama na maziwa, kuendesha mafunzo na mashamba darasa ya mifugo na kilimo. Wataalamu hawa ofisi zao zipo kwenye ofisi za vijiji na kata. Wananchi wanahamasishwa kuwatumia ili waweze  kuzalisha kitaalamu.

9.0  MIUNDOMBINU YA MIFUGO

Miundombinu iliyopo ni kama ifuatavyo:

No.
MIUNDOMBINU
IDADI ZILIZOPO
ZINAZOFANYA KAZI
INAYOHITAJI MATENGENEZO
1
Vituo vya matibabu ya Mifugo
2
1
1
2
Minada
1
1

3
Majosho
7
6
1
5
Malambo
1
1
-
6
Machinjio
2
2
-
7
Maeneo ya kuwamba ngozi
1
2
1
1
-
2
8
Vituo vya kusindika maziwa
2
2
0
9
Shamba darasa la malisho
1
1
-

 

10. CHANGAMOTO

Ukosefu wa maeneo ya kutosha ya malisho na maji kwa Mifugo ukilinganisha na Idadi ya Mifugo iliyopo.

  • Mabadiliko ya tabia nchi yanayosababisha vifo vya Mifugo kwa ukame pamoja na  milipuko ya magonjwa kama Bondela Ufa, Sotoka ya mbuzi na kondoo na Kimeta.
  • Upungufu wa wataalamu wa Mifugo.
  • Bajeti ndogo ya kusimamia na kuendeleza sekta ya mifugo.
  • Kukosekana kwa soko la ngozi  ambapo hadi sasa kuna vipande zaidi ya 8,000.vya ngozi ya ng’ombe.
  • Uvamizi wa mifugo  toka Wilaya za jirani na hata nchi jirani kutafuta malisho katika eneo la NARCO.

11. MIKAKATI

1  .Kuhamasisha wafugaji kuvuna ili kubaki na mifugo Michache iliyo bora.

2.  Kutoa elimu kwa wafugaji juu ya Ufugaji bora Wenye tija, kuboresha nyanda za malisha na kutunza vyanzo vya maji.

3.  Kutoa elimu kwa njia ya ziara za mafunzo na kuhudhuria maonyesho mbalimbali.

4. kuhamasisha wafugaji kuchangia gharama za kinga,tiba na shughuli za maendeleo ya mifugo.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA WALIOITWA KAZINI SIHA DC OKTOBA 2024 October 21, 2024
  • TANGAZO LA KOSEGEZWA MBELE UKODISHAJI WA MASHAMBA January 22, 2025
  • TANGAZO NAFASI YA MWENYEKITI BODI YA AJIRA HALMASHAURI YA SIHA KILIMANJARO February 18, 2025
  • TANGAZO NAFASI ZA KAZI SIHA August 28, 2020
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • Rais Samia aendelea kuitangaza Tanzania Kimataifa

    April 11, 2025
  • Rais Samia aendelea kuitangaza Tanzania Kimataifa

    April 11, 2025
  • Uzinduzi Sera ya Ardhi Siha yashiriki

    March 17, 2025
  • Umoja wa Ulaya kuendelea kushirikiana na Tanzania

    March 12, 2025
  • Ona Zote

Video

WATUMISHI SIHA DC WAASWA KUFANYA KAZI KWA UADILIFU
Video zingine

Viunganisho vya haraka

  • Wasifu wa Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Wasifu wa Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri
  • Soma taarifa zote ndani ya tovuti
  • Blog ya Halmashauri
  • facebook ya Halmashauri
  • Matokeo ya Taifa Darasa la Saba 2016 Siha
  • kuomba pasipoti kupitia mtandaoni
  • WARAKA WA MAVAZI KWA WATUMISHI WA UMMA
  • Fomu za Likizo Watumishi wa Umma

Viunganisho Vinavyohusiana

  • Basic Education Statistics
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Takwimu za taifa
  • Idara ya habari maelezo
  • tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Wananchi Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotazama

free HitCounter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji,Halmashauri ya Wilaya ya Siha /Siha District Council

    sanduku la Posta: 5 BR- Sanya Juu -Elerai S.L.P 129, 25482 SIHA

    simu: 0272-970677

    Mobile: 0713164432 DED Siha

    Email: ded@sihadc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani Ya eneo

Copyright ©2017 SihaDistrictCouncil . All rights reserved.