• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Serikali |
    • Malalamiko |
Siha District Council
Siha District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serekali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Siha

  • Mwanzo
  • Historia
    • Dhima na Dira
    • Wasifu wa Wilaya
  • Utawala
    • Muundo wa Kiutawala
    • Idara
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Kilimo,Ushirika na Umwagiliaji
      • Idara ya Mipango,Takwimu na Umwagiliaji
      • Idara ya Elimu Msingi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
    • Kata
      • Sanya Juu
      • Gararagua
      • Karansi
      • Biriri
      • Songu
      • Makiwaru
      • Olkolili
      • Ormelili
      • DonyoMuruak
      • Ngarenairobi
      • Ndumet
      • Mitimirefu
      • Livishi
      • Nasai
      • Kirua
      • Kashashi
      • Ivaeny
  • Huduma zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za maji
    • huduma za Watumishi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Tourism
  • Machapisho
    • Fomu za Maombi
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria
    • Jarida Mtandaoni Kila mwezi
  • Kituo cha habari
    • Maktaba ya Picha
    • Videos
    • Hutuba
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Elimu,Afya na Maji
      • Ujenzi,Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
      • Wajumbe Mkutano wa ALAT
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba vikao 2022/2023
    • Ratiba M/Kiti Halmashauri

Wananchi Siha na Wadau Wafanikiwa Kuudhibiti Moto Uliozuka Ranchi ya NARCO - West Kilimanjaro

Posted on: August 19th, 2024

Wananchi wa Wilaya ya Siha kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wamefanikiwa kuudhibiti moto mkubwa uliozuka Agosti 18, 2024 majira ya Saa Saba Mchana katika Ranchi ya Taifa ya West Kilimanjaro na kuteketeza robo ya eneo la malisho ya mifugo.

Akizungumza leo wakati wa kuangalia eneo lililoathiriwa na kufanya tathmini ya maafa yaliyojitokeza kwa wananchi na wawekezaji Agosti 19, 2024 Meneja wa Ranchi ya Taifa ya West Kilimanjaro Raymond Lutege amesema eneo lililoungua linakadiriwa kufikia hekari 7827 na sehemu kubwa ni eneo linalotumiwa na wananchi kwa malisho pamoja na Mwekezaji wa Kampuni ya Tanzania Game and Livestock breeders.

Meneja Lutege amemshukuru Mkuu wa Wilaya ya Siha Mhe. Dkt Christopher Timbuka kwa kutafuta wadau waliosaidiana na Jeshi la Polisi na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kilimanjaro kuzima moto ili usisababishe athari kubwa zaidi.

“Tunamshukuru sana pia Mbunge wa Jimbo la Siha Mhe. Dkt Godwin Mollel na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha Dkt Haji Mnasi kwa kuwahamasisha wananchi wanaoishi maeneo jirani na Ranchi ya Taifa ya West Kilimanjaro kushirikiana nasi kuzima moto huo” amesema Meneja Lutege.

Amesema kupitia hamasa za viongozi wa vijiji jirani wananchi walijitokeza kwa wingi kushirikiana nasi kuzima moto huo ambao ulidhibitiwa majira ya Saa Nne Usiku wa kuamkia leo.

“Eneo kubwa lililoathirika ni eneo la vitalu vya wafugaji, ifahamike kuwa Ranchi ya West Kilimanjaro tuna jumla ya vitalu saba, na katika vitalu saba tumebaki na vitalu viwili na nusu ambavyo havikupata madhara ya moto” ameongeza Meneja Lutege.

Meneja wa Ranchi ya Taifa ya West Kilimanjaro Raymond Lutege amesema kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama wanaendelea kuchunguza chanzo cha moto huo na hatua zaidi zitachukuliwa kudhibiti matukio kama hayo kujitokeza.

Meneja wa Ranchi ya Taifa ya West Kilimanjaro Raymond Lutege leo Agosti 19, 2024 akimuonesha Katibu Tarafa wa Siha Magharibi Janeth Jonas Obedy maeneo yaliyoathirika na moto wakati wa kuangalia eneo lililoathiriwa na kufanya tathmini ya maafa yaliyojitokeza kwa wananchi na wawekezaji.

Muonekano wa eneo la Ranchi ya Taifa ya West Kilimanjaro lililoungua na  moto mkubwa uliozuka Agosti 18, 2024 majira ya Saa Saba Mchana katika Ranchi hiyo na kuteketeza robo ya eneo la malisho ya mifugo.


Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA WALIOITWA KAZINI SIHA DC OKTOBA 2024 October 21, 2024
  • TANGAZO LA KOSEGEZWA MBELE UKODISHAJI WA MASHAMBA January 22, 2025
  • TANGAZO NAFASI YA MWENYEKITI BODI YA AJIRA HALMASHAURI YA SIHA KILIMANJARO February 18, 2025
  • TANGAZO NAFASI ZA KAZI SIHA August 28, 2020
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • Rais Samia aendelea kuitangaza Tanzania Kimataifa

    April 11, 2025
  • Rais Samia aendelea kuitangaza Tanzania Kimataifa

    April 11, 2025
  • Uzinduzi Sera ya Ardhi Siha yashiriki

    March 17, 2025
  • Umoja wa Ulaya kuendelea kushirikiana na Tanzania

    March 12, 2025
  • Ona Zote

Video

WATUMISHI SIHA DC WAASWA KUFANYA KAZI KWA UADILIFU
Video zingine

Viunganisho vya haraka

  • Wasifu wa Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Wasifu wa Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri
  • Soma taarifa zote ndani ya tovuti
  • Blog ya Halmashauri
  • facebook ya Halmashauri
  • Matokeo ya Taifa Darasa la Saba 2016 Siha
  • kuomba pasipoti kupitia mtandaoni
  • WARAKA WA MAVAZI KWA WATUMISHI WA UMMA
  • Fomu za Likizo Watumishi wa Umma

Viunganisho Vinavyohusiana

  • Basic Education Statistics
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Takwimu za taifa
  • Idara ya habari maelezo
  • tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Wananchi Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotazama

free HitCounter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji,Halmashauri ya Wilaya ya Siha /Siha District Council

    sanduku la Posta: 5 BR- Sanya Juu -Elerai S.L.P 129, 25482 SIHA

    simu: 0272-970677

    Mobile: 0713164432 DED Siha

    Email: ded@sihadc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani Ya eneo

Copyright ©2017 SihaDistrictCouncil . All rights reserved.