• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Serikali |
    • Malalamiko |
Siha District Council
Siha District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serekali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Siha

  • Mwanzo
  • Historia
    • Dhima na Dira
    • Wasifu wa Wilaya
  • Utawala
    • Muundo wa Kiutawala
    • Idara
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Kilimo,Ushirika na Umwagiliaji
      • Idara ya Mipango,Takwimu na Umwagiliaji
      • Idara ya Elimu Msingi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
    • Kata
      • Sanya Juu
      • Gararagua
      • Karansi
      • Biriri
      • Songu
      • Makiwaru
      • Olkolili
      • Ormelili
      • DonyoMuruak
      • Ngarenairobi
      • Ndumet
      • Mitimirefu
      • Livishi
      • Nasai
      • Kirua
      • Kashashi
      • Ivaeny
  • Huduma zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za maji
    • huduma za Watumishi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Tourism
  • Machapisho
    • Fomu za Maombi
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria
    • Jarida Mtandaoni Kila mwezi
  • Kituo cha habari
    • Maktaba ya Picha
    • Videos
    • Hutuba
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Elimu,Afya na Maji
      • Ujenzi,Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
      • Wajumbe Mkutano wa ALAT
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba vikao 2022/2023
    • Ratiba M/Kiti Halmashauri

USIMAMIZI MIRADI YA MAENDELEO, UKUSANYAJI MAPATO NI LAZIMA – BI MWAMBETA

Posted on: July 29th, 2025

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha Bi. Hellen Mwambeta amewahimiza watendaji wa kata na vijiji kusimamia kikamilifu miradi ya maendeleo na ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri ili kuleta maendeleo kwa wananchi.

Bi. Hellen Mwambeta ametoa rai hiyo leo Julai 29, 2025 wakati akihitimisha kikao cha mafunzo elekezi ya matumizi ya mfumo wa usimamizi wa utendaji kazi katika utumishi wa umma (PEPMIS) na mfumo wa TAUSI kwa watendaji wa Kata na Vijiji yaliyofanyika katika ukumbi mkubwa wa mikutano wa makao makuu ya Halmashauri.

Amewasihi watendaji wa kata na vijiji kufanya ufuatiliaji karibu, usimamizi na wabunifu wa nyanzo vipya vya mapato ili kupanua wigo wa ukusanyaji na kuhakikisha hakuna upotevu wa mapato katika maeneo wanayoyasimamia.

“Tuimarishe vyanzo vilivyopo vya mapato na kuzuia uharibifu unaoweza kujitokeza ili kiendelee kuiletea Halmashauri mapato na kubuni vyanzo vipya vya mapato vilivyopo katika vijiji na kata” amesema Mkurugenzi Mtendaji Bi. Hellen Mwambeta.

Pia amewasisitiza watendaji kusimamia kwa ukaribu miradi ya maendeleo na kuwashirikisha wananchi kuanzia mwanzo wa mradi hadi unapokamilika kwa kuwasomea matumizi ya fedha za miradi kwenye vikao vya kata na vijiji.

Aidha, Bi. Mwambeta amesema bila ushirkiano wa watendaji wa vijiji na kata, timu ya menejimenti na jamii husika kunakwamisha shughuli za maendeleo hivyo kila mmoja anatakiwa kuwa tayari kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na kwa kushirikiana.

“Kwa hiyo Naomba tukawajibike, na tukazingatie sheria, kanuni na miongozo ili kufanikisha shughuli za maendeleo kwa wanananchi” amesema Mkurugenzi Mtendaji Bi. Hellen Mwambeta.

“Pia naomba tuwe waaminifu kwenye kusimamia miradi ya maendeleo, ukusanyaji wa mapato na mambo mengine yote ya kiutendaji, ukiwa na uaminifu na uadilifu utakuwepo, kwa hiyo tufanye kazi kwa uaminifu na uadilifu mkubwa” ameongeza Bi. Mwambeta. 

Kikao cha mafunzo elekezi ya matumizi ya mfumo wa usimamizi wa utendaji kazi katika utumishi wa umma (PEPMIS) na mfumo wa TAUSI kwa watendaji wa Kata na Vijiji kimefanyika ili kuongeza ufanisi na uwajibikaji wakati wa utekelezaji wa shughuli za serikali.

Wajumbe wa kikao cha mafunzo elekezi ya matumizi ya mfumo wa usimamizi wa utendaji kazi katika utumishi wa umma (PEPMIS) na mfumo wa TAUSI kwa watendaji wa Kata na Vijiji kilichofanyika leo Julai 29, 2025 katika ukumbi mkubwa wa mikutano wa makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Siha

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA WALIOITWA KAZINI SIHA DC OKTOBA 2024 October 21, 2024
  • TANGAZO NAFASI YA MWENYEKITI BODI YA AJIRA HALMASHAURI YA SIHA KILIMANJARO February 18, 2025
  • TANGAZO NAFASI ZA KAZI SIHA DC JUNI 2025 June 10, 2025
  • TANGAZO NAFASI ZA KAZI SIHA August 28, 2020
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • Menejimenti SIHA DC yaendelea Ukaguzi miradi

    July 30, 2025
  • Menejimenti SIHA DC yaendelea Ukaguzi miradi

    July 30, 2025
  • USIMAMIZI MIRADI YA MAENDELEO, UKUSANYAJI MAPATO NI LAZIMA – BI MWAMBETA

    July 29, 2025
  • SIHA IPO TAYARI MAONESHO NANE NANE 2025

    July 28, 2025
  • Ona Zote

Video

WATUMISHI SIHA DC WAASWA KUFANYA KAZI KWA UADILIFU
Video zingine

Viunganisho vya haraka

  • Wasifu wa Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Wasifu wa Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri
  • Soma taarifa zote ndani ya tovuti
  • Blog ya Halmashauri
  • facebook ya Halmashauri
  • Matokeo ya Taifa Darasa la Saba 2016 Siha
  • kuomba pasipoti kupitia mtandaoni
  • WARAKA WA MAVAZI KWA WATUMISHI WA UMMA
  • Fomu za Likizo Watumishi wa Umma

Viunganisho Vinavyohusiana

  • Basic Education Statistics
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Takwimu za taifa
  • Idara ya habari maelezo
  • tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Wananchi Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotazama

free HitCounter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji,Halmashauri ya Wilaya ya Siha /Siha District Council

    sanduku la Posta: 5 BR- Sanya Juu -Elerai S.L.P 129, 25482 SIHA

    simu: 0272-970677

    Mobile: 0713164432 DED Siha

    Email: ded@sihadc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani Ya eneo

Copyright ©2017 SihaDistrictCouncil . All rights reserved.