• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Serikali |
    • Malalamiko |
Siha District Council
Siha District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serekali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Siha

  • Mwanzo
  • Historia
    • Dhima na Dira
    • Wasifu wa Wilaya
  • Utawala
    • Muundo wa Kiutawala
    • Idara
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Kilimo,Ushirika na Umwagiliaji
      • Idara ya Mipango,Takwimu na Umwagiliaji
      • Idara ya Elimu Msingi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
    • Kata
      • Sanya Juu
      • Gararagua
      • Karansi
      • Biriri
      • Songu
      • Makiwaru
      • Olkolili
      • Ormelili
      • DonyoMuruak
      • Ngarenairobi
      • Ndumet
      • Mitimirefu
      • Livishi
      • Nasai
      • Kirua
      • Kashashi
      • Ivaeny
  • Huduma zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za maji
    • huduma za Watumishi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Tourism
  • Machapisho
    • Fomu za Maombi
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria
    • Jarida Mtandaoni Kila mwezi
  • Kituo cha habari
    • Maktaba ya Picha
    • Videos
    • Hutuba
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Elimu,Afya na Maji
      • Ujenzi,Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
      • Wajumbe Mkutano wa ALAT
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba vikao 2022/2023
    • Ratiba M/Kiti Halmashauri

TAMBUA MRADI WA BOOST UTAKAVYOBORESHA SEKTA YA ELIMU

Posted on: December 30th, 2022

 

NINI MAANA YA BOOST

BOOST ni  Mradi wa kuimarisha Ufundishaji na Ujifunzaji  kwa Shule za  Awali na Msingi Tanzania Bara  BOOST  ni sehemu ya Mpango wa Lipa Kulingana na Matokeo  EP4R  na inachangia utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Sekta ya Elimu  kwa miaka mitano 2021/2022 hadi 2026.

 

MATOKEO MUHIMU YA MRADI WA BOOST

Vyumba vipya vya Madarasa 12 kujengwa na vifaa vya Shule vinavyohusika katika maeneo yenye uhitaji Zaidi.

Vituo 800 katika Shule za Msingi/Vituo  vya Walimu kuanzishwa na kuendelezwa kwa ajili ya utoaji wa mafunzo kwa njia ya TEHAMA kupitia maktaba mtandao /kielektroniki na mfumo wa usimamizi wa ujifunzaji kimtandao.

Shule za Msingi 6000 kuwezeshwa kutekeleza programu ya Shule ya Msingi salama

Madarasa 12,000 ya Elimu ya Awali yaliyoboreshwa pamoja na njia bora za ufundishaji vikiwemo vifaa vya ujifunzaji

Kuongezeka kwa uwiano wa uandikishaji wa wanafunzi wa Elimu ya Awali kutoka asilimia 57.5 hadi asilimia 85.

VIASHIRIA VITAKAVYO PIMWA

Mradi wa BOOST unafuata utaratibu wa ufadhili unaozingatia Lipa kulingana na matokeo ,kwa hivyo utoaji wa fedha unatategemea  kufikiwa kwa matokeo yaliyokubaliwa kama yatakavyothibitishwa na Wakala Huru aliyeajiriwa chini ya Mpango huu. Jumla ya viashiria 8 na viwango vyake vya ufadhili vimebainishwa hapa chini:

 

AFUA 1: UTEKELEZAJI WA MPANGO WA UENDELEZAJI WA MIUNDOMBINU YA SHULE UNAOZINGATIA MAHITAJI

 hii inasimamiwa na Mhandisi wa Halmashauri , Afisa Elimu Msingi na  Afisa Elimu Vifaa na Takwimu.

                                                      

LENGO LA AFUA NAMBA -1   ni kuboresha miundombinu katika Shule za Msingi

Mpango huu utabainisha mahitaji na kuweka mpango wa ujenzi , mpango huo utajumuisha ukarabati na  upanuzi wa shule zilizopo pamoja na ujenzi wa Shule mpya za Awali na Msingi katika maeneo ya kimkakati . Mwongozo wa ujenzi wa shule pia utahuishwa ili kuimarisha viwango vya ubora ,usalama na manunuzi.

Halmashauri itapata pesa kutokana na jinsi itakavyo maliza Mradi kwa wakati na kwa kufuata  Kanuni ,  Miongozo na utaratibu .

 

AFUA NAMBA 2 UTEKELEZAJI WA MPANGO WA SHULE ZA MSINGI SALAMA

AFUA NAMBA 2:  Ina shughulikiwa na Afisa Ustawi wa Jamii, Afisa Maendeleo ya Jamii na Afisa Elimu msingi.

Mpango wa Shule Salama ni Mpango ambao umelenga kupunguza vikwazo vya Elimu kwa watoto wote hasa walemavu ili waweze kumaliza mzunguko wa Elimu na kutimiza ndoto zao.

Lengo la Mpango wa Shule salama ni Kuboresha mazingira ya kufundisha na kujifunzia ili kuwajengea wanafunzi  uwezo wa Kujihamini ,Kujieleza, Kujitambua na Kujilinda dhidi ya changamoto mbalimbali

  • Kumwezesha Mwalimu kutambua maadili ya kazi yake.
  • Kuhimarisha mahusihano kati ya Shule na Jamii.
  • Kuweka mazingiraa ya mapito salama kwa Wanafunzi kwenda Shuleni na kurudi nyumbani.

VIGEZO VITAKAVYO PIMWA

  • Mapitio ya Mpango wa Maendeleo wa Shule kama umewekwa utaratibu wa utekelezaji wa Mpango wa Shule za Msingi Salama.
  • Muhtasari wa vikaoo vya Kamati ya Shule je , wanajadili utekelezaji wa Mpango wa Shule salama
  • Kuwepo na taratibu shuleni za kuzuia utoro na kumfanya motto apende shule kama vile uwepo wa chakula shuleni, Club mbalimbali shuleni kama vile Tuseme uwepo wa Bendi ya Shule
  • Kuwepo kwa mazingira  ya  mapito salama kwa Wanafunzi wanapopita kwenda Shuleni na kurudi nyumbani  .
  • Uwepo wa Dawati maalum Shuleni la kushughulikia malalamiko ya wanafunzi
  • Kila Shule iwe na kumbukumbu ya malalamiko na jinsi yalivyo fanyiwa kazi                                                                                     

AFUA NAMBA 3

KUONGEZEKA KWA ASILIMIA YA UWIANO WA UANDIKISHAJI WA WANAFUNZI WA ELIMU YA AWALI.

 

LENGO LA AFUA HII

 Kuimarisha Madarasa ya Elimu ya Awali Nchini .

Mhusika ni Afisa Elimu Msingi,Afisa Elimu Vifaa na Takwimu na Mhandisi

 

VIGEZO VITAKAVYOPIMWA

  • Ongezeko la Uandikishaji wa Wanafunzi wa Darasa la  Awali kwa asilimia 100

Halmashauri inahimizwa kubuni mikakati ya kuongeza uandikishaji wa Wanafunzi katika madarasa ya Elimu ya Awali

AFUA NAMBA 4

UTEKELEZAJI WA NJIA BORA NA MATUMIZI YA VIFAA STAHIKI VYA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA KATIKA MADARASA YA ELIMU YA AWALI.

Lengo la Afua hii ni kuboresha mazingira ya Ujifunzaji na Ufundishaji kwa wanafunzi wa darasa la Awali kwa kutumia zana katika ufundishaji ili kumfanya mtoto apende shule na aweze kuelewa mada kwa urahisi.

MHUSIKA 

 Afisa Elimu Taaluma na Afisa Elimu vifaa na Takwimu.

 

VIGEZO VITAKAVYO PIMWA

  • Uwepo wa Vifaa vya kufundisha na kujifunzia vinavyoendana na umri wa watoto na viwe vya kufurahisha na kuongeza maarifa.
  • Kuandaa Miongozo ya Elimu ya Awali ili kumsaidia mwalimu kwenda kufundisha vema.
  • Uwepo wa vitabu vya hadithi za watoto.
  • Uwepo wa Vitabu vya shughuli za watoto kwani watoto wanajifunza Zaidi kwa matendo .
  • Uwepo wa Vichezeo vya watoto vinavyo endana na Mazingira na Mukitadha.

AFUA NAMBA 5. 

HALMASHAURI ZINATEKELEZA MAFUNZO ENDELEVU YA WALIMU KAZINI (MEWEKA) KATIKA NGAZI ZA SHULE NA KUPITIA VITUO VYA WALIMU.

MEWAKA ni mpango wa mafunzo endelevu  ya walimu kazini ambapo ngazi kuu ya utekelezaji ni shule ikisaidiwa na Vituo  vya  Walimu ambavyo vimeboreshwa kwa kuwa na vifa mbalimbali vikiwemo vifaa vya TEHAMA .

MHUSIKA

Katika AFUA hii mhusika ni Afisa Elimu Taaluma

 

LENGO LA AFUA HII

Lengo la AFUA ya MEWAKA Kuongeza nguvu za utekelezaji wa Walimu Shuleni  kuboresha mazingira ya ufundishaji na ufundishaji shuleni.Walimu wataunda vikundi vidogovidogo vya kujisomea kwa kumtumia Mwalimu mahiri katika somo  husika  shuleni

-Kuwaongezea Walimu ujuzi wawepo kazini ili mwalimu anapokutana na changamoto shuleni kuweza kuzitatua katika ngazi ya Shule zikishindikana hapeleke ngazi ya Kata zikishindikana halite ngazi ya Halmashauri.

VIGEZO VITAKAVYO PIMWA 

  • Halmashauri inatakiwa kuweka bajeti ya MEWAKA kila mwaka
  • Ratiba ya MEWAKA iwepo shuleni
  • Kalenda ya MEWAKA
  • Mahudhurio ya Walimu
  • Form za tathimini
  • Mada watakazo jadili
  • Mpango kazi wa MEWAKA uwepo shuleni.

 AFUA NAMBA 6

IDADI YA SHULE ZA MSINGI NA VITUO VYA WALIMU (TRC) VINAVYOTEKELEZA MTAALA WA TEHAMA  KATIKA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA VINAVYOWEZESHWA KUPITIA MFUMO WA USIMAMIZI WA UJIFUNZAJI

 

MHUSIKA

Mhusika katika AFUA hii ni Afisa Elimu Taaluma na Afisa Elimu Takwimu na Vifaa.

LENGO LA AFUA HII

Lengo kuu ni kuwa na angalau Shule moja ya Msingi katika kila Kata nchini Tanzania inayotekeleza mpango wa mafunzo ya TEHAMA ili kusaidia utekelezaji wa MEWAKA na ufundishaji na ujifunzaji.

 

LENGO MAHUSUSI

  • Kumjengea Mwalimu umahiri katika matumizi ya TEHAMA wakati wa wa ufundishaji
  • Kila Mwanafunzi ifikapo 2025 awe anaweza kutumia TEHAMA katika kujifunza

VIGEZO VITAKAVYOPIMWA

  • Uwepo wa mwongozo wa somo la TEHAMA Shuleni
  • Idadi ya walimu na wanafunzi waliopata mafunzo ya TEHAMA na wanatumia komputa
  • Jengo lenye vifaa vya TEHAMA
  • Uwepo wa vifaa vya TEHAMA
  • Uwepo wa Miundombinu rafiki ,chumba maalum cha TEHAMA


  • AFUA NAMBA 7
  • UTENGAJI WA BAJETI KWA AJILI YA KUWEZESHA  SHUGHULI MUHIMU ZA PROGRAMU NA KUHAKIKISHA KUWA KIWANGO CHA BAJETI KINADUMISHWA AU KUONGEZWA  
  • MHUSIKA
  • Mhusika katika AFUA hii ni Afisa Mipango na Mkaguzi wa ndani.
  • LENGO LA AFUA HII
  • ni Kuboresha mapokezi na matumizi bora ya matumizi ya fedha za mradi wa BOOST.
  •  
  • MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KATIKA AFUA HII
  • AFUA zetu zote ziingizwe  kwenye Bajeti  ili pesa za mradi zisikose kifungu
  • Matumizi ya fedha za mradi zinatumika kwa kuzingatia kanuni, taratibu  na miongozo ya Serikali
  • Kuhakikisha kitengo cha ukaguzi wa ndani kufanya ukaguzi wa mradi na matumizi ya fedha za mradi
  • Kuhakikisha kuwa hesabu za mradi zinawakilishwa kwa CAG kwa ukaguzi na nyaraka zote ziwe wazi
  • Manunuzi ya vifaa vya mradi yafuate kanuni na taratibu za manunuzi
  • Kutoa taarifa za mapato na matumizi kwa wakati
  • Kutunza kumbukumbu zote za mradi kwa usahihi.
  • VIGEZO VYA UPIMAJI
  • Uwepo wa bajeti mfano bajeti ya ujenzi wa miundombinu  Mpya na ukarabati
  • Miongozo  ya matumizi ya fedha
  • Taarifa ya mradi
  • Manunuzi ya vifaa na matumizi yake
  • Uwepo wa taarifa ya mapato na matumizi
  •       
  • AFUA NAMBA 8 
  • IDADI YA HALMASHAURI ZINAZOKIDHI VIGEZO VYA UTAWALA BORA KATIKA ELIMU 
  • LENGO LA MRADI
  • Kuimarishwa kwa Utawala Bora Katika sekta ya elimu
  • Kuhakikisha vigezo vya utawala bora vinazingatiwa Shuleni.
  • MHUSIKA ni Afisa Elimu Msingi, Afisa Elimu Taaluma, Afisa Elimu Vifaa na Takwimu, Waratibu Elimu Kata, na Walimu wakuu Shule za Msingi.  
  • Mwongozo wa utawala Bora katika Elimu  Utajumisha uwekaji wa mipango , usimamizi wa Shule, ukaguzi wa ndani, usimamizi wa ujenzi, ushirikishwaji wa jamii  na ushughulikiaji  wa malalamiko
  • VIGEZO VITAKAVYOPIMWA 
  • Kuwepo kwa miongozo ya uongozi na utawala bora
  • Kiwango cha ushirikishwaji wa jamii katika shughuli za  Shule
  • Kujumuisha Mipango ya Shule katika Mipango ya Halmashauri
  • Uwepo wa Kamati za Shule
  • Uwepo wa Shule zitakazo kaguliwa na Mkaguzi wa fedha wa ndani
  • Uwepo wa taarifa za mkaguzi wa ndani kwenye majalada 
  • Uwepo wa taarifa za ufuatiliaji na tathimini za robo Mwaka, nusu Mwaka na Mwaka.

Imeandaliwa na 

                             Timu Boost Halmashauri ya Wilaya ya Siha-Kilimanjaro

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA WALIOITWA KAZINI SIHA DC OKTOBA 2024 October 21, 2024
  • TANGAZO LA KOSEGEZWA MBELE UKODISHAJI WA MASHAMBA January 22, 2025
  • TANGAZO NAFASI YA MWENYEKITI BODI YA AJIRA HALMASHAURI YA SIHA KILIMANJARO February 18, 2025
  • TANGAZO NAFASI ZA KAZI SIHA August 28, 2020
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • Rais Samia aendelea kuitangaza Tanzania Kimataifa

    April 11, 2025
  • Rais Samia aendelea kuitangaza Tanzania Kimataifa

    April 11, 2025
  • Uzinduzi Sera ya Ardhi Siha yashiriki

    March 17, 2025
  • Umoja wa Ulaya kuendelea kushirikiana na Tanzania

    March 12, 2025
  • Ona Zote

Video

WATUMISHI SIHA DC WAASWA KUFANYA KAZI KWA UADILIFU
Video zingine

Viunganisho vya haraka

  • Wasifu wa Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Wasifu wa Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri
  • Soma taarifa zote ndani ya tovuti
  • Blog ya Halmashauri
  • facebook ya Halmashauri
  • Matokeo ya Taifa Darasa la Saba 2016 Siha
  • kuomba pasipoti kupitia mtandaoni
  • WARAKA WA MAVAZI KWA WATUMISHI WA UMMA
  • Fomu za Likizo Watumishi wa Umma

Viunganisho Vinavyohusiana

  • Basic Education Statistics
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Takwimu za taifa
  • Idara ya habari maelezo
  • tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Wananchi Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotazama

free HitCounter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji,Halmashauri ya Wilaya ya Siha /Siha District Council

    sanduku la Posta: 5 BR- Sanya Juu -Elerai S.L.P 129, 25482 SIHA

    simu: 0272-970677

    Mobile: 0713164432 DED Siha

    Email: ded@sihadc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani Ya eneo

Copyright ©2017 SihaDistrictCouncil . All rights reserved.