• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Serikali |
    • Malalamiko |
Siha District Council
Siha District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serekali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Siha

  • Mwanzo
  • Historia
    • Dhima na Dira
    • Wasifu wa Wilaya
  • Utawala
    • Muundo wa Kiutawala
    • Idara
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Kilimo,Ushirika na Umwagiliaji
      • Idara ya Mipango,Takwimu na Umwagiliaji
      • Idara ya Elimu Msingi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
    • Kata
      • Sanya Juu
      • Gararagua
      • Karansi
      • Biriri
      • Songu
      • Makiwaru
      • Olkolili
      • Ormelili
      • DonyoMuruak
      • Ngarenairobi
      • Ndumet
      • Mitimirefu
      • Livishi
      • Nasai
      • Kirua
      • Kashashi
      • Ivaeny
  • Huduma zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za maji
    • huduma za Watumishi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Tourism
  • Machapisho
    • Fomu za Maombi
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria
    • Jarida Mtandaoni Kila mwezi
  • Kituo cha habari
    • Maktaba ya Picha
    • Videos
    • Hutuba
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Elimu,Afya na Maji
      • Ujenzi,Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
      • Wajumbe Mkutano wa ALAT
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba vikao 2022/2023
    • Ratiba M/Kiti Halmashauri

DED SIHA AMPONGEZA MHE. RAIS KWA UWEKEZAJI MKUBWA SEKTA YA ELIMU

Posted on: January 31st, 2024

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha Haji Mnasi, PhD ameupongeza uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali ya awamu ya Sita Chini ya uongozi wa Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika sekta ya elimu kwa lengo la kuboresha ujifunzaji na ufundishaji.

Mnasi, PhD ametoa pongezi hizo leo January 31, 2024 wakati akifungua kikao kazi na wakuu wa shule za sekondari kilichofanyika katika shule ya sekondari ya wasichana Kilimanjaro ambapo amesema serikali imeweka mikakati inayohakikisha elimu ya sekondari inatolewa kwa ubora na ufanisi ili malengo ya nchi ya kuwa na raia walioelimika.

Amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa katika sekta ya elimu hasa katika halmashauri ya wilaya ya siha huku akiwataka viongozi katika sekta hiyo kumsaidia kwa kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

"Niendelee kumshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo anaendelea kuitendea haki sekta hii ya elimu hasa katika halmashauri yetu ya Wilaya ya Siha, sisi tuendelee kumsaidia kwa kutimiza wajibu wetu" amesema Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Siha Haji Mnasi, PhD.

Akizungumzia ufaulu wa wanafunzi wa kidato cha nne mwaka 2023, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha Haji Mnasi, PhD ameipongeza Divisheni ya Elimu Sekondari na Wakuu wa Shule kwa jitihada zilizofanyika kwa mwaka 2023 zilizosaidia kupandisha ufaulu kutoka asilimia 88 kwa mwaka 2022 hadi asilimia 92 mwaka 2023 hali inayoashiria kuwa uwezo wa kufikia asilimia 100 iwapo nguvu na mikakati zaidi itaongezwa.

“Kwanza niwapongeze kwa matokeo ya mitihani ya kidato cha nne mwaka 2023, kumekuwa na mjongeo chanya wa matokeo kutoka asilimia 88 mwaka 2022 hadi 92 kwa mwaka 2023, hii ni ishara ya wazi kwamba tunaweza kufikia asilimia 100 iwapo nguvu na jitihada zaidi zitaongezwa kwa kuweka mikakati bora ya ufundishaji” amesema Mnasi.

 “Matokeo haya mazuri ya kidato cha nne yametokana na jitihada na vikao mkakati mlivyofanya na kutekeleza yale mnayokubaliana katika kuhakikisha Mnaboresha elimu na kupandisha ufaulu katika Shule zetu za sekondari” ameongeza Mkurugenzi Mtendaji Mnasi.

Amewaagiza Wakuu wa Shule kujielekeza kutafakari na kujadili ufundishaji unamlenga mwanafunzi mmoja mmoja, ujenzi wa umahirikupitia wanafunzi kupatiwa nyenzo muhimu za kufikiri, kutenda na kupenda masomo, shule kuwa na mazingira salama, tulivu na yanayohamasisha wanafunzi kujifunza na ufuatiliaji wa karibu wa ufundishaji na ujifunzaji.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA WALIOITWA KAZINI SIHA DC OKTOBA 2024 October 21, 2024
  • TANGAZO LA KOSEGEZWA MBELE UKODISHAJI WA MASHAMBA January 22, 2025
  • TANGAZO NAFASI YA MWENYEKITI BODI YA AJIRA HALMASHAURI YA SIHA KILIMANJARO February 18, 2025
  • TANGAZO NAFASI ZA KAZI SIHA August 28, 2020
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • MILIONI 316.5 YATOLEWA KWA VIKUNDI 48 WILAYANI SIHA

    May 23, 2025
  • Mchengerwa awapongeza Maofisa Habari Nchini Kwa uchapa kazi

    May 23, 2025
  • Mchengerwa awapongeza Maofisa Habari Nchini Kwa uchapa kazi

    May 23, 2025
  • Mchengerwa awapongeza Maofisa Habari Nchini Kwa uchapa kazi

    May 23, 2025
  • Ona Zote

Video

WATUMISHI SIHA DC WAASWA KUFANYA KAZI KWA UADILIFU
Video zingine

Viunganisho vya haraka

  • Wasifu wa Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Wasifu wa Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri
  • Soma taarifa zote ndani ya tovuti
  • Blog ya Halmashauri
  • facebook ya Halmashauri
  • Matokeo ya Taifa Darasa la Saba 2016 Siha
  • kuomba pasipoti kupitia mtandaoni
  • WARAKA WA MAVAZI KWA WATUMISHI WA UMMA
  • Fomu za Likizo Watumishi wa Umma

Viunganisho Vinavyohusiana

  • Basic Education Statistics
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Takwimu za taifa
  • Idara ya habari maelezo
  • tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Wananchi Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotazama

free HitCounter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji,Halmashauri ya Wilaya ya Siha /Siha District Council

    sanduku la Posta: 5 BR- Sanya Juu -Elerai S.L.P 129, 25482 SIHA

    simu: 0272-970677

    Mobile: 0713164432 DED Siha

    Email: ded@sihadc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani Ya eneo

Copyright ©2017 SihaDistrictCouncil . All rights reserved.