• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Serikali |
    • Malalamiko |
Siha District Council
Siha District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serekali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Siha

  • Mwanzo
  • Historia
    • Dhima na Dira
    • Wasifu wa Wilaya
  • Utawala
    • Muundo wa Kiutawala
    • Idara
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Kilimo,Ushirika na Umwagiliaji
      • Idara ya Mipango,Takwimu na Umwagiliaji
      • Idara ya Elimu Msingi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
    • Kata
      • Sanya Juu
      • Gararagua
      • Karansi
      • Biriri
      • Songu
      • Makiwaru
      • Olkolili
      • Ormelili
      • DonyoMuruak
      • Ngarenairobi
      • Ndumet
      • Mitimirefu
      • Livishi
      • Nasai
      • Kirua
      • Kashashi
      • Ivaeny
  • Huduma zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za maji
    • huduma za Watumishi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Tourism
  • Machapisho
    • Fomu za Maombi
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria
    • Jarida Mtandaoni Kila mwezi
  • Kituo cha habari
    • Maktaba ya Picha
    • Videos
    • Hutuba
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Elimu,Afya na Maji
      • Ujenzi,Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
      • Wajumbe Mkutano wa ALAT
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba vikao 2022/2023
    • Ratiba M/Kiti Halmashauri

TAARIFA YA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA SIHA BARAZA LA MADIWANI TAREHE 7/FEBRUARI/2018

07 February 2018

OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

HALMASHAURI YA WILAYA YA SIHA




TAARIFA YA MWENYEKITI WA HALMASHAURI MKUTANO WA KAWAIDA WA BARAZA LA MADIWANI KATIKA KIPINDI CHA ROBO YA KWANZA (OKTOBA -DESEMBA,2017).

Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Siha,

Mwakilishi Ofisi ya RAS-Mkoa wa Kilimanjaro,

Mh. Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Siha,

Mh. Kaimu Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Siha,

Waheshimiwa Madiwani,

Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Siha,

Viongozi wa Dini,

Wageni Waalikwa,

Ndugu Wataalamu,

Waandishi wa Habari,

Wananchi wa Wilaya ya Siha,

Mabibi na Mabwana,

 

Hongereni na Sikukuu Krismass na mwaka mpya 2018,nategemea kuwa wote mpo wazima wa afya tele. Naomba tusimame kwa dakika moja kuwakumbuka wale wote waliotangulia mbele ya haki kwa mwaka 2017

 

 

 

Wah. Madiwani , na Ndugu Wananchi,

Awali ya yote napenda kumshukuru Mungu kwa kutupatia uzima na amani katika mwaka huu wa 2018,Pili napenda kuwakaribisha tena Waheshimiwa Madiwani,Wananchi,Wadau wa Maendeleo,Wataalam wa Halmashauri na Waandishi wa Habari katika Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Wah. Madiwani katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2017/2018 (Oktoba hadi Desemba,2017). Kipekee napenda kumshukuru Mungu kwa kwa kutupatia nguvu na maono ya kutosha katika kuwatumikia wananchi wa Siha.

A)SEKTA YA KILIMO NA MIFUGO

Napenda kuwakumbusha Wananchi wa Wilaya ya Siha kuwa sasa tunaingia katika kipindi cha kuanza maandalizi ya kuandaa mashamba kwa ajili ya msimu mkubwa wa mvua za masika ambao kimsingi tumezoea msimu unaanza mwishoni mwa mwezi huu au mapema mwezi Machi.

Naomba wataalam wa Kilimo katika Wilaya yetu waliopo katika ngazi ya Kata na Vijiji watusaidia kuwahimiza wananchi kulima kilimo kinachozingatia sayansi ili kuongeza wingi wa mazao na hatimaye kuboresha kipato. Najua kwa dunia ya leo kilimo ni sayansi kwani kilimo kisichozingatia utaalam, kipato chake ni kidogo sana,hivyo natoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa wataalam wa kilimo na kuzingatia maelekezo na ushauri unaotolewa na wataalam hao.

Aidha katika sekta ya Mifugo,nimepewa taarifa kuwa, zoezi la upigaji chapa ng’ombe katika Halmashauri yetu limekamilika kwa mafanikio makubwa. Zoezi hilo lilianza rasmi mwezi Novemba,2017 na kumalizika tarehe 31/01/2018 ambapo zaidi ya ng’ombe 25,735 wamepigwa chapa ambayo ni sawa na asilimia 84 ya lengo ya kupiga chapa ng’ombe 30,527 waliopo katika Wilaya yetu.

Naomba kutoa pongezi na shukrani za dhati kwa Wananchi na wakazi wote wa Wilaya ya Siha kwa ushirikiano walionesha kufanikisha zoezi hili muhimu ambapo ni agizo la Serikali yetu. Vilevile napenda kutoa pongezi kwa Ofisi ya Mkurugenzi pamoja na wataalam wote kwa jinsi walivyojituma na kusimamia zoezi hili hadi kufikia mafanikio makubwa tuliyonayo. Nimeambiwa kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Siha ni miongoni mwa Halmashauri zilizofanya vizuri katika Mkoa wa Kilimanjaro,hongereni sana.

(B)UKUSANYAJI WA MAPATO

Waheshimiwa Madiwani, Ndugu Wananchi

Pamoja na kuwa,Halmashauri yetu inakabiliwa na tatizo kubwa la kuwa na vyanzo vichache na vya uhakika vya mapato ya ndani, lakini mimi kama Mwenyekiti napenda tuchukue changamoto hii kuwa fursa ya kujikwamua. Nimepewa taarifa kuwa hali ya ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa miezi ya mwisho wa mwaka 2017 pamoja na mwezi Januari 2018 imeongezeka kwa kiasi kikubwa hasa mapato yanayotokana leseni. Naomba kutoa wito kwa Waheshimiwa Madiwani kuendelea kutoa ushirikiano wa kusimamia mianya yote inayosababisha upotevu wa mapato ya ndani ya Halmashauri yetu. Naomba kutoa wito kwa idara inayohusika na ukusanyaji wa mapato kuhakikisha kuwa mashine za kieletroniki za kukusanyia mapato zinanunuliwa za kutosha ikiwezekana kila makusanyo yafanywe kupitia mashine hizo kama ilivyo agizo la Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pia natoa agizo kwa Mkurugenzi Mtendaji kuendelea kuwachukulia hatua zinazostahiki watendaji wote wa Umma watakaoshindwa kusimamia kikamilifu suala zima la ukusanyaji wa mapato.Hapa hatutakuwa na mchezo kabisa kwani kushindwa kukusanya mapato kutasababisha halmashauri kushindwa kutoa hutuma kwa wananchi wake.

(C) UTUNZAJI WA MAZINGIRA 

Waheshimiwa Madiwani,ndugu Wananchi .

Napenda kuchukua fursa hii kuwaomba Wananchi na wakazi wote wa Siha kushiriki vema katika kupanda miti wakati msimu wa mvua za masika utakapoanza na upandaji huo wa miti nashauri uzingatie miti ambayo haisababishi ukame na kukausha vyanzo vyetu vya maji. Narudia tena kuwaagiza Watendaji wetu wa Vijiji na Kata pamoja na maofisa kilimo kuwasaidia wananchi kuwapa ushauri bora wa aina ya miti ya kuotesha hasa wakati huu msimu wa mvua unapokaribia.

Ni ukweli usiopingika kuwa miti katika Wilaya yetu imepungua sana hata kuanza kuhatarisha hali ya baadhi ya maeneo kuwa jangwa jambo ambalo halikuwepo miaka 20 iliyopita. Naomba kutoa wito kwa viongozi wenzangu kuendelea kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira kwa wananchi na wakazi wa Wilaya ya Siha popote pale tunapopata nafasi ya kuongea na Wananchi na kama ikiwezekana sisi viongozi kuwa mfano wa jambo hilo.

(D)SEKTA YA ELIMU

Kwanza kabisa nianze kwa kutoa pongezi nyingi kwa Wilaya yetu ya Siha kufanya vizuri katika matokeo ya kidato cha Nne 2017 yaliyotangazwa hivi karibuni,ambapo katika matokeo hayo Halmashauri ya Siha imeshika nafasi ya Pili mkoa wa Kilimanjaro na nafasi 16 kitaifa. Napenda tena kuwapongeza walimu wote wa shule za sekondari kwa kufanya kazi yao vizuri na hatimaye kuongeza ufaulu katika shule zetu. Naomba wananchi na wakazi wa Siha tuendelee kutoa ushirikiano kwa wataalam wetu hawa kwa manufaa ya watoto wetu na jamii kwa ujumla. Nimepata taarifa kuwa matokeo ya kidato cha pili pia yametoka na hali ya ufaulu kwa shule zetu ni ya kuridhisha.

Aidha, kwa upande wa shule za msingi bado hatufanyi vizuri sana kutokana na changamoto mbalimbali zinazotukabili ikiwemo ya uchakavu wa miundombinu katika shule nyingi za msingi. Naomba wazazi,wananchi na viongozi tushirikiane na Serikali katika kupunguza kama siyo kumaliza changamoto hii katika shule zetu za msingi. Sambamba na miundombinu pia tunalo tatizo la utoro mashuleni,ukosefu wa chakula pamoja na ukosefu wa mahitaji mengine muhimu kwa watoto wetu.

Vilevile , lipo tatizo la nidhamu mbaya kwa baadhi ya shule inayooneshwa na watoto wetu kwa walimu mashuleni pamoja na mimba za utotoni,naomba wazazi kwa pamoja tushirikiane kwa lengo la kuinua kiwango cha ufaulu kwa shule zetu. Naomba tena kuwaomba waheshimiwa madiwani tushirikiane kwa pamoja kusimamia shule zetu kwani kwa kufanya hivyo tutakuwa tumeisadia jamii yetu kwa kiasi kikubwa sana.

Taarifa nilizonazo ni kuwa,ufaulu katika shule za msingi Wilaya ya Siha umepanda na kufikia asilimia 72.76 mwaka 2017 kutoka asilimia 70.36 mwaka 2016. Naomba tukaze buti zaidi ili walau tufikie asilimia zaidi ya 80 kwa mwaka huu 2018.

(E) SEKTA YA AFYA

Napenda kuwashukuru wale wote walioshiriki katika kufanikisha ujenzi wa wodi ya kinamama katika hospital yetu ya Wilaya ya Siha,naona maendeleo ya ujenzi huo yanaendelea vizuri na yapo katika hatua za mwisho za ukamilishwaji wake na baada ya kukamilika wananchi wetu wanaanza kupata huduma bora. Naomba kuwakumbusha tena wadau,wananchi na sisi sote tuliotoa ahadi ya kuchangia ujenzi huo tujitahidi kukamilisha michango yetu kwa wakati ili kufikia malengo yalitarajiwa. Taarifa nilizonazo ni kuwa hadi Januari 2018 uchangiaji ulikuwa kama ifuatavyo:- Jumla ya ahadi zilizotolewa ni shilingi 136,105,000/=,Fedha taslimu shilingi 78,537,000/= na vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya Tshs. 37,835,000/=. Kipekee naomba kuishukuru ofisi ya Mkuu wetu wa Wilaya ya Siha kwa jinsi ilivyoweza kufuatilia kwa karibu jambo hili lenye manufaa kwa Wananchi wa Siha,hongera sana mhe. Mkuu wetu wa Wilaya ya Siha,Mimi kama Mwenyekiti wa Halmashauri ya Siha pamoja na baraza la Madiwani tunapenda kukuhakikishia kuwa tupo pamoja katika shughuli zote za maendeleo pamoja na zile za kijamii kwa lengo moja tu la maendeleo ya Wananchi wa Wilaya ya Siha.

Vilevile nimeambiwa kuwa ukamilishwaji wa ujenzi wa jengo la ghorofa moja kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa wa nje lipo katika hatua za mwisho mwisho na hivi karibuni huduma zitaanza kutolewa katika hospital yetu ya Wilaya husasani huduma za upasuaji. Napenda kuishukuru Serikali yetu ya Tanzania kwa kutupatia fedha shilingi milioni 250 zilizosaidia kufanya kazi hiyo. Vilevile nimeambiwa kuwa hali ya upatikanaji wa dawa katika Zahanati na vituo vya afya Wilayani Siha ni nzuri na ni matumaini yangu kuwa hali hiyo itazidi kuwa nzuri zaidi kwa siku za baadaye.

Naomba tena kuwaomba wadau wa maendeleo,Wananchi na viongozi wenzangu kuendelea na moyo wa kuchangia shughuli za maendeleo bila kujali itikadi zetu za kisiasa,imani zetu za Dini au bila kujali maeneo tunayotoka,wote sisi ni Watanzania tushirikiane kwa umoja wetu.

Waheshimiwa Madiwani,Ndugu Wananchi;

Napenda kuwaomba wananchi wote wa Halmashauri ya Siha wakati huu shule zimeshafunguliwa tujitahidi kuhakikisha kuwa watoto wote wanaostahili kuwa shuleni wanakwenda bila kubaki hata mmoja na tushirikiane kukomesha utoro katika shule zetu za msingi na sekondari. Naomba viongozi wote kwa umoja wetu tusaidiane ili kufanikisha jambo hili. Naomba kwa hili kumwagiza Mkurugenzi mtendaji Halmashauri ya Siha kupitia watendaji wake wa vijiji na Kata kusimamia kudhibiti utoro mashuleni ili kuongeza ufaulu wa wanafunzi katika shule za Siha.

Waheshimiwa Madiwani na ndg Wananchi;

Kabla ya kufika mwisho wa Taarifa yangu, napenda kuwashukuru tena Wananchi wa Wilaya ya Siha na Waheshimiwa Madiwani kwa ushirikiano wenu wa dhati mnaoendelea kunipatia kwa ajili ya kutekeleza majukumu yangu ya Kila siku. Pia napenda wote kwa pamoja tumshukuru Mungu kwa kumaliza mwaka wa fedha 2017 kwa salama na kuingia mwaka mpya wa 2018. Naomba wote kwa umoja wetu tufanye kazi kwa kushirikiana ili kuharakisha maendeleo yetu pamoja na maendeleo ya familia zetu , Wilaya ya Siha ,Mkoa wa Kilimanjaro na Taifa kwa ujumla wake.

Mwisho kabisa ,nichukue fursa hii kwa niaba ya baraza la Madiwani, kuwashukuru tena kwa usikivu wenu mkubwa mlionesha tangu mwanzo wa taarifa yangu, naomba usikivu na utulivu huu uendelee hadi mwisho wa Mkutano wetu na hatimaye tumalize na kuagana kwa upendo na furaha.

Asanteni sana kwa kunisikiliza

Imetolewa na:


Frank K. Tarimo

Mwenyekiti wa Halmashauri (W)

SIHA

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA WALIOITWA KAZINI SIHA DC OKTOBA 2024 October 21, 2024
  • TANGAZO LA KOSEGEZWA MBELE UKODISHAJI WA MASHAMBA January 22, 2025
  • TANGAZO NAFASI YA MWENYEKITI BODI YA AJIRA HALMASHAURI YA SIHA KILIMANJARO February 18, 2025
  • TANGAZO NAFASI ZA KAZI SIHA August 28, 2020
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • Rais Samia aendelea kuitangaza Tanzania Kimataifa

    April 11, 2025
  • Rais Samia aendelea kuitangaza Tanzania Kimataifa

    April 11, 2025
  • Uzinduzi Sera ya Ardhi Siha yashiriki

    March 17, 2025
  • Umoja wa Ulaya kuendelea kushirikiana na Tanzania

    March 12, 2025
  • Ona Zote

Video

WATUMISHI SIHA DC WAASWA KUFANYA KAZI KWA UADILIFU
Video zingine

Viunganisho vya haraka

  • Wasifu wa Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Wasifu wa Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri
  • Soma taarifa zote ndani ya tovuti
  • Blog ya Halmashauri
  • facebook ya Halmashauri
  • Matokeo ya Taifa Darasa la Saba 2016 Siha
  • kuomba pasipoti kupitia mtandaoni
  • WARAKA WA MAVAZI KWA WATUMISHI WA UMMA
  • Fomu za Likizo Watumishi wa Umma

Viunganisho Vinavyohusiana

  • Basic Education Statistics
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Takwimu za taifa
  • Idara ya habari maelezo
  • tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Wananchi Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotazama

free HitCounter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji,Halmashauri ya Wilaya ya Siha /Siha District Council

    sanduku la Posta: 5 BR- Sanya Juu -Elerai S.L.P 129, 25482 SIHA

    simu: 0272-970677

    Mobile: 0713164432 DED Siha

    Email: ded@sihadc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani Ya eneo

Copyright ©2017 SihaDistrictCouncil . All rights reserved.