• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Serikali |
    • Malalamiko |
Siha District Council
Siha District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serekali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Siha

  • Mwanzo
  • Historia
    • Dhima na Dira
    • Wasifu wa Wilaya
  • Utawala
    • Muundo wa Kiutawala
    • Idara
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Kilimo,Ushirika na Umwagiliaji
      • Idara ya Mipango,Takwimu na Umwagiliaji
      • Idara ya Elimu Msingi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Tehama
      • Uchaguzi
      • Nyuki
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
    • Kata
      • Sanya Juu
      • Gararagua
      • Karansi
      • Biriri
      • Songu
      • Makiwaru
      • Olkolili
      • Ormelili
      • DonyoMuruak
      • Ngarenairobi
      • Ndumet
      • Mitimirefu
      • Livishi
      • Nasai
      • Kirua
      • Kashashi
      • Ivaeny
  • Huduma zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za maji
    • huduma za Watumishi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Tourism
  • Machapisho
    • Fomu za Maombi
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria
  • Kituo cha habari
    • Maktaba ya Picha
    • Videos
    • Hutuba
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi iliyokamilika
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Elimu,Afya na Maji
      • Ujenzi,Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
      • Wajumbe Mkutano wa ALAT
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba vikao 2018/2019
    • Ratiba M/Kiti Halmashauri

Wasifu wa Wilaya

UTANGULIZI

Halmashauri ya Wilaya ya Siha ilianzishwa rasmi tarehe 01.07.2007 kwa sheria No 7 ya mwaka 1982 .na kuwa miongoni mwa Wilaya Sita za Mkoa wa Kilimanjar,Wilaya nyingine ni Rombo,Same,Mwanga,Hai na Moshi. Wilaya ya Siha ina Jimbo moja la uchaguzi, Tarafa 5 nazo ni Siha Magharibi,Siha Kati,Siha Mashariki,Siha Kusini na Siha Kaskazini.Wilaya pia inazo Kata 17,Vijiji 60 na Vitongoji 169.

Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 Wilaya ya Siha inajumla wa watu 116,313 wanaume wakiwa 56,500 na Wanawake wakiwa 59,813.

MIPAKA 

Wilaya ya Siha inakadiriwa kuwa kati ya nyuzi za Longitudi 37.3”-37.17’’ upande wa mashariki na Latitudi 2.5’’ hadi 3.00’’ kusini. Wilaya ya Siha inajumla wa ukubwa wa eneo ya mraba 1158 na Wilaya imepakana na Wilaya ya Hai upande wa Kusini,Wilaya ya Longido na Rombo upande Kaskazini Magharibi,Wilaya ya Meru na Hai upande wa Kusini Mashariki.Upande wa Mashariki imepakana na hifadhi ya mlima Kilimanjaro.

Wilaya ya Siha ina Makabila zaidi ya 125 wengi wakiwa ni wachagga,Wamasai na Makabila mengine yaliyopo. Shughuli kubwa za kiuchumi kwa wananchi na wakazi wa Wilaya ya Siha ni kilimo na ufugaji ambapo watu wachache wanajishughulisha na biashara ndogo ndogo na biashara za kati.

UTAWALA

Wilaya ya Siha imeundwa kwa Utawala kuanzia ngazi ya Serikali kuu Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Halmashauri ya Wilaya. Kwa upande wa Halmashauri utawala umepangwa kuanzia baraza la Madiwani,Mkurugenzi Mtendaji,Wakuu wa Idara na Vitengo,Maofisa na Watumishi wengine wa serikali kuanzia ngazi ya Makao makuu hadi watumishi waliopo ngazi ya Vijiji na Kata. Halmashauri ya Wilaya ya Siha inajumla ya watumishi wa Umma 1269 wengi wa watumishi hawa wakiwa ni sekta ya Elimu na Afya

SHUGHULI ZA KIUCHUMI

Wananchi na wakazi wengi wanaoishi katika Wilaya ya siha wanafanya shughuli za Kilimo na Ufugaji katika kuinua kiwango cha uchumi kuanzia ngazi ya Kaya,Kijiji,Kata,hadi Wilaya. Mazao makuu ya chakula yanayolimwa katika Wilaya ya Siha ni pamoja na Maharagwe,Mahindi,Viazi, Mbaazi,Ndizi na mazao ya mboga mboga. Aidha Mazao ya biashara yanayolimwa katika Wilaya ya Siha ni pamoja na Kahawa,Shairi,Ngano,Parachichi na Miti ya Mbao katika shamba la miti West Kilimanjaro.

UWEKEZAJI NA VIVUTIO VYA UTALII

Wilaya ya Siha ni miongoni mwa Wilaya chache katika mkoa wa Kilimanjaro zenye mashamba makubwa na yenye rutuba yaliyopo katika maeneo mazuri yenye kupata mvua za kutosha mara mbili kwa mwaka kutoka kilele cha mlima Kilimanjaro. Mashamba haya yamekuwa chanzo kikubwa cha kuendeleza kilimo cha mazao ya biashara na yale ya chakula yanayosafirishwa nje ya Wilaya ya siha na kusaidia kuongeza mapato ya ndani ya Halmashauri kupitia utozaji wa ushuru wa mazao hayo.

Aidha, Watalii wengi wanaopanda mlima kilimanjaro kupita lango la Londorosi hadi shira platu hupitia katika vijiji na vitongoji mbalimbali vya wilaya ya Siha na kujionea tamaduni mbalimbali za Wananchi na wakazi wa Siha. Wilaya ya Siha pia inayo mboga ndogo ya wanyama Pori (Ndarakwai) kando kando mwa njia inayopanda mlima Kilimanjaro. Hifadhi hii ndogo ya wanyama imekuwa kivutio kikubwa kwa watalii kupitia Wilaya ya Siha wakati wanapanda mlima Kilimanjaro.

HUDUMA ZA KIJAMII

a) AFYA 

Wilaya ya Siha inajumla ya Hospital 2,moja hospital ya taifa ya kifua kikuu na hospitali ya Wilaya ya Siha,Vituo vya afya 5, kimoja cha Serikali na vituo 4 vya mashirika ya dini,Zahanati 14 ,9 za Serikali na 6 za mashirika ya Dini na watu binafsi. Hali ya upatikanaji wa huduma za Afya ni wa kuridhisha na wananchi wengi wanapata huduma za afya kwa wakati na karibu na maeneo wanayoishi.

b) b)MAJI 

Hali ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika Wilaya ya Siha hadi mwishoni mwa mwaka 2017 ni asilimia 86,ambapo wananchi na wakazi wengi wa wilaya ya Siha hupata maji ya bomba kwa umbali chini ya mita 400. Kwa ujumla Wilaya ya Siha ni miongoni mwa wilaya chache hapa nchini zinazowapatia wananchi wake huduma ya maji ya uhakika katika siku 7 za wiki masaa 24 ndani ya siku 365 za mwaka.

c) ELIMU

Wilaya ya Siha inajumla ya shule 19 za Sekondari,13 za Serikali na 5 za Mashirika ya Dini.Karibu kata zote za Wilaya ya siha zina shule za sekondari za Wazazi ambapo wanafunzi hutembea umbali chini ya kilomita 4 kufika shule husika.hali ya miundombinu ya shule za sekondari ni ya kuridhisha.

Kwa upande wa elimu msingi,Wilaya ya Siha inajumla ya shule 59,53 za Serikali na 6 za mashirika ya dini na binafsi. Kila mwanafunzi wa shule za msingi na sekondari amepatiwa dawati la kukaa akiwa darasani. Hali ya utoaji wa elimu katika Wilaya ya Siha ni ya kuridhisha kwani watoto wote wa shule za msingi na sekondari wanapata chakula cha mchana wakiwa mashuleni

Matangazo

  • HOTUBA YA RAIS KULIHUTUBIA BUNGE LA 12 TAREHE 13 NOVEMBA 2020 November 13, 2020
  • TANGAZO LA VIBALI VYA UJENZI SIHA January 22, 2021
  • TANGAZO VIWANJA SIHA 2021 January 21, 2021
  • TANGAZO LA MKUTANO WA KAWAIDA BARAZA LA WAH. MADIWANI H.W SIHA KIPINDI CHA ROBO YA KWANZA(JULAI HADI SEPTEMBA 2017) November 24, 2017
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • Serikali yaendelea na zoezi tokomeza Nzige Siha

    February 24, 2021
  • Mafunzo ya Mfumo wa picha kwa Watahiniwa yatolewa kwa Walimu SIHA

    February 19, 2021
  • Serikali yatoa Milioni 210 Maabara 7 za Sekondari Siha

    February 13, 2021
  • Zahanati Roseline,Sinai na Messe zapatiwa fedha za ujenzi na Serikali

    February 12, 2021
  • Ona Zote

Video

Siha yapogezwa ujenzi kituo cha Polisi
Video zingine

Viunganisho vya haraka

  • Wasifu wa Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Wasifu wa Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri
  • Soma taarifa zote ndani ya tovuti
  • Blog ya Halmashauri
  • facebook ya Halmashauri
  • Matokeo ya Taifa Darasa la Saba 2016 Siha
  • kuomba pasipoti kupitia mtandaoni
  • WARAKA WA MAVAZI KWA WATUMISHI WA UMMA
  • Fomu za Likizo Watumishi wa Umma

Viunganisho Vinavyohusiana

  • Basic Education Statistics
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Takwimu za taifa
  • Idara ya habari maelezo
  • tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Wananchi Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotazama

free HitCounter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Sanya Juu-Siha Kilimanjaro

    sanduku la Posta: S.L.P 129 Sanya Juu

    simu: 027-2970677

    Mobile: 0622643108

    Email: ded@sihadc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani Ya eneo

Copyright ©2017 SihaDistrictCouncil . All rights reserved.