• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Serikali |
    • Malalamiko |
Siha District Council
Siha District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serekali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Siha

  • Mwanzo
  • Historia
    • Dhima na Dira
    • Wasifu wa Wilaya
  • Utawala
    • Muundo wa Kiutawala
    • Idara
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Kilimo,Ushirika na Umwagiliaji
      • Idara ya Mipango,Takwimu na Umwagiliaji
      • Idara ya Elimu Msingi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
    • Kata
      • Sanya Juu
      • Gararagua
      • Karansi
      • Biriri
      • Songu
      • Makiwaru
      • Olkolili
      • Ormelili
      • DonyoMuruak
      • Ngarenairobi
      • Ndumet
      • Mitimirefu
      • Livishi
      • Nasai
      • Kirua
      • Kashashi
      • Ivaeny
  • Huduma zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za maji
    • huduma za Watumishi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Tourism
  • Machapisho
    • Fomu za Maombi
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria
    • Jarida Mtandaoni Kila mwezi
  • Kituo cha habari
    • Maktaba ya Picha
    • Videos
    • Hutuba
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Elimu,Afya na Maji
      • Ujenzi,Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
      • Wajumbe Mkutano wa ALAT
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba vikao 2022/2023
    • Ratiba M/Kiti Halmashauri

Waziri wa Afya afanya ziara Wilaya ya Siha

Posted on: October 5th, 2024

Taarifa ya Ziara ya Waziri wa Afya, Mhe. Jenista Mhagama - Wilaya ya Siha, Mkoa wa Kilimanjaro


Tarehe 5 Oktoba 2024, Waziri wa Afya, Mhe. Jenista Mhagama, alifanya ziara katika Wilaya ya Siha, Mkoa wa Kilimanjaro, akilenga kuboresha huduma za afya katika Zahanati ya Mawasiliano na Hospitali ya Magonjwa Ambukizi Kibong'oto. Ziara hii ilihusisha tathmini ya huduma zinazotolewa na kuangazia changamoto zinazokabili zahanati na hospitali hizo.


Katika Zahanati ya Mawasiliano iliyopo kijiji cha Mawasiliano  Kata ya Gararagua, Waziri Mhagama alikagua miundombinu na huduma zinazotarajiwa kutolewa mara baada ya kufunguliwa.

 Alisisitiza umuhimu wa kuboresha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba ili kuhakikisha jamii inapata huduma bora za afya. Alitoa maelekezo ya kuimarisha ushirikiano kati ya zahanati na hospitali kubwa za rufaa ili kuboresha mnyororo wa huduma za afya.


Akiwa katika Zahanati ya Mawasiliano mhe.Mhagama alifanya Harambee ndogo iliyowezesha kupatikana kwa Fedha za kujenga kibanda cha kukaa wagonjwa wakati wasubiri kupata huduma mbalimbali katika Zahanati hiyo.

Akiwa Mawasiliano Mhe.Mhagana aliweka jiwe la Msingi la Zahanati ya Mawasiliano na kupongeza uongozi wa Wilaya ya Siha pamoja na Halmashauri ya Siha kwa usimamizi bora wa  ujenzi wa Zahanati hiyo.


Waziri Mhagama alitembelea Hospitali ya Magonjwa Ambukizi Kibong'oto, ambapo alikagua idara mbalimbali na kuzungumza na wafanyakazi wa afya. Alisisitiza umuhimu wa kuimarisha elimu ya afya kwa jamii kuhusu magonjwa ambukizi, pamoja na kuwataka wahudumu wa afya kuendelea na mafunzo ya kitaaluma ili kuboresha huduma.


Waziri Mhagama pia alizungumza kuhusu changamoto zinazowakabili waganga wa TB kutoka migodi ya Mererani, Mkoa wa Manyara. Aliweka wazi mpango wa Serikali wa kuwasaidia waganga hao kwa kutoa elimu na vifaa vya kupimia na kutibu TB. Alitaja umuhimu wa kushirikiana na wadau wa maendeleo ili kufanikisha kampeni za uhamasishaji kuhusu kinga na matibabu ya TB, pamoja na kuanzisha vituo vya afya karibu na maeneo ya kazi.

Ziara hii ililenga kuimarisha huduma za afya na kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora, huku akihimiza umuhimu wa ushirikiano katika kufanikisha malengo ya afya katika jamii. Mhe. Mhagama aliahidi kufuatilia maendeleo ya mipango iliyowekwa ili kuhakikisha utekelezaji wa ahadi hizo.


Katika ziara ya Waziri wa Afya, Mhe. Jenista Mhagama, alibainisha kuwa Serikali inatumia rasilimali kubwa katika kuwahudumia wagonjwa wa TB. Kila mwaka, Serikali inatumia takriban shilingi bilioni 10 kwa ajili ya matibabu, uchunguzi, na usaidizi wa kifaa kwa wagonjwa wa TB. Hii ni pamoja na gharama za dawa, vifaa vya uhamasishaji, na elimu kwa umma.

Kuhusu umri unaoathirika zaidi na ugonjwa huu, kundi lililo katika hatari kubwa ni watu wenye umri kati ya miaka 15 hadi 49. Hata hivyo, watoto na wazee pia wako katika hatari ya kupata TB, hasa katika maeneo yenye maambukizi makubwa. Mhe. Mhagama alisisitiza umuhimu wa kutoa elimu kwa makundi haya ili kupunguza maambukizi na kuhakikisha matibabu yanapatikana kwa wakati.

Aliahidi kuwa Serikali itapanua mikakati ya kupunguza mzigo wa TB nchini, ikishirikiana na wadau wa ndani na nje ya Nchi.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA WALIOITWA KAZINI SIHA DC OKTOBA 2024 October 21, 2024
  • TANGAZO LA KOSEGEZWA MBELE UKODISHAJI WA MASHAMBA January 22, 2025
  • TANGAZO NAFASI YA MWENYEKITI BODI YA AJIRA HALMASHAURI YA SIHA KILIMANJARO February 18, 2025
  • TANGAZO NAFASI ZA KAZI SIHA August 28, 2020
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • Rais Samia aendelea kuitangaza Tanzania Kimataifa

    April 11, 2025
  • Rais Samia aendelea kuitangaza Tanzania Kimataifa

    April 11, 2025
  • Uzinduzi Sera ya Ardhi Siha yashiriki

    March 17, 2025
  • Umoja wa Ulaya kuendelea kushirikiana na Tanzania

    March 12, 2025
  • Ona Zote

Video

WATUMISHI SIHA DC WAASWA KUFANYA KAZI KWA UADILIFU
Video zingine

Viunganisho vya haraka

  • Wasifu wa Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Wasifu wa Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri
  • Soma taarifa zote ndani ya tovuti
  • Blog ya Halmashauri
  • facebook ya Halmashauri
  • Matokeo ya Taifa Darasa la Saba 2016 Siha
  • kuomba pasipoti kupitia mtandaoni
  • WARAKA WA MAVAZI KWA WATUMISHI WA UMMA
  • Fomu za Likizo Watumishi wa Umma

Viunganisho Vinavyohusiana

  • Basic Education Statistics
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Takwimu za taifa
  • Idara ya habari maelezo
  • tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Wananchi Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotazama

free HitCounter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji,Halmashauri ya Wilaya ya Siha /Siha District Council

    sanduku la Posta: 5 BR- Sanya Juu -Elerai S.L.P 129, 25482 SIHA

    simu: 0272-970677

    Mobile: 0713164432 DED Siha

    Email: ded@sihadc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani Ya eneo

Copyright ©2017 SihaDistrictCouncil . All rights reserved.