• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Serikali |
    • Malalamiko |
Siha District Council
Siha District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serekali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Siha

  • Mwanzo
  • Historia
    • Dhima na Dira
    • Wasifu wa Wilaya
  • Utawala
    • Muundo wa Kiutawala
    • Idara
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Kilimo,Ushirika na Umwagiliaji
      • Idara ya Mipango,Takwimu na Umwagiliaji
      • Idara ya Elimu Msingi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
    • Kata
      • Sanya Juu
      • Gararagua
      • Karansi
      • Biriri
      • Songu
      • Makiwaru
      • Olkolili
      • Ormelili
      • DonyoMuruak
      • Ngarenairobi
      • Ndumet
      • Mitimirefu
      • Livishi
      • Nasai
      • Kirua
      • Kashashi
      • Ivaeny
  • Huduma zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za maji
    • huduma za Watumishi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Tourism
  • Machapisho
    • Fomu za Maombi
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria
    • Jarida Mtandaoni Kila mwezi
  • Kituo cha habari
    • Maktaba ya Picha
    • Videos
    • Hutuba
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Elimu,Afya na Maji
      • Ujenzi,Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
      • Wajumbe Mkutano wa ALAT
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba vikao 2022/2023
    • Ratiba M/Kiti Halmashauri

Wanaochangia utoro wa wanafunzi Mashuleni waonywa:DC Siha

Posted on: April 10th, 2019

Mkuu wa Wilaya ya Siha Mhe. Onesmo Buswelu amewataka wazazi na walezi katika Wilaya ya Siha kuwapatia elimu watoto wakike na wale wa kiume bila kuwabagua kwa misingi ya jinsia zao.

Hayo ameyasema akiwa katika shule ya Sekondari Matadi iliyopo Kata ya Ndumet Tarafa ya Siha Magharibi aliposhiriki na wananchi katika ujenzi wa madarasa mawili unaoendelea shuleni hapo. Ndugu zangu wananchi wa Ndumet leo nimefika hapa kushirikiana nanyi katika shughuli za maendeleo hasa ujenzi wa madarasa mawili unaoendelea shuleni hapa alisema Buswelu.

Aliwaeleza wananchi kuwa Serikali ya Tanzania inayoongozwa na Mhe. Rais Magufuli imewaletea shilingi milioni 25 katika shule ya sekondari Matadi kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa vyumba viwili vya Madarasa vilivyoanzishwa kwa nguvu za wananchi wa Kata ya Ndumet.

Hata hivyo Mhe. Buswelu akiwa shuleni hapo alitoa agizo kwa viongozi wote kuanzia ngazi ya Kata,Vijiji hadi vitongoji kusimamia kwa karibu mahudhurio ya wanafunzi mashuleni na pale itapoonekana watoto wa shule wanajishuhulisha na kazi za mashambani muda na wakati wa siku za shule basi wazazi /walezi husika wachukuliwe hatua kali za kisheria.

Ndugu zangu kwa hili la utoro mashuleni nitachukua hatua mara moja kwa wale wote watakaohusika kwani watu hao ni maadui wakubwa wa maendeleo ya Wilaya ya Siha na Taifa kwa ujumla alisema Mhe. Buswelu.

Naye Diwani wa Kata ya Ndumet Mhe. Jackson Rabo alisema kuwa Wananchi wa Kata ya Ndumet wamefurahi sana kwa Serikali kutoa kiasi cha milioni 25 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi huo, Kwa niaba yangu binafsi na kwa niaba ya Viongozi wa Kata na Vijiji tunapenda kuishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mhe. Rais wetu mpendwa Magufuli kwa jinsi anavyotujali wananchi wanyonge kama sisi alisema Rabo.

Halmashauri ya Wilaya ya Siha Mkoa wa Kilimanjaro katika kipindi cha mwaka 2019 imepokea jumla ya shilingi milioni 200 kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa miradi viporo wa madarasa (maboma) katika shule mbalimbali ya Sekondari za Serikali Wilayani Siha.

Mkuu wa Wilaya ya Siha Mhe. Onesmo Buswelu (katikati) akishiriki katika kazi ya ujenzi katika shule ya sekondari Matadi


Mkuu wa Wilaya ya Siha Mhe. Onesmo Buswelu(aliyebeba ndoo ya maji) akionesha mfano wa viongozi kushirikiana na wananchi katika kazi za maendeleo,


Wananchi  na mafundi mbalimbali wakishiriki katika kazi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa Katika shule ya sekondari Matadi Kata ya Ndumet


Wanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya Sekondari Matadi wakiwa darasani kwa ajili ya kuhudhuria vipindi vya kila siku shuleni hapo

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA WALIOITWA KAZINI SIHA DC OKTOBA 2024 October 21, 2024
  • TANGAZO LA KOSEGEZWA MBELE UKODISHAJI WA MASHAMBA January 22, 2025
  • TANGAZO NAFASI YA MWENYEKITI BODI YA AJIRA HALMASHAURI YA SIHA KILIMANJARO February 18, 2025
  • TANGAZO NAFASI ZA KAZI SIHA August 28, 2020
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • Rais Samia aendelea kuitangaza Tanzania Kimataifa

    April 11, 2025
  • Rais Samia aendelea kuitangaza Tanzania Kimataifa

    April 11, 2025
  • Uzinduzi Sera ya Ardhi Siha yashiriki

    March 17, 2025
  • Umoja wa Ulaya kuendelea kushirikiana na Tanzania

    March 12, 2025
  • Ona Zote

Video

WATUMISHI SIHA DC WAASWA KUFANYA KAZI KWA UADILIFU
Video zingine

Viunganisho vya haraka

  • Wasifu wa Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Wasifu wa Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri
  • Soma taarifa zote ndani ya tovuti
  • Blog ya Halmashauri
  • facebook ya Halmashauri
  • Matokeo ya Taifa Darasa la Saba 2016 Siha
  • kuomba pasipoti kupitia mtandaoni
  • WARAKA WA MAVAZI KWA WATUMISHI WA UMMA
  • Fomu za Likizo Watumishi wa Umma

Viunganisho Vinavyohusiana

  • Basic Education Statistics
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Takwimu za taifa
  • Idara ya habari maelezo
  • tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Wananchi Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotazama

free HitCounter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji,Halmashauri ya Wilaya ya Siha /Siha District Council

    sanduku la Posta: 5 BR- Sanya Juu -Elerai S.L.P 129, 25482 SIHA

    simu: 0272-970677

    Mobile: 0713164432 DED Siha

    Email: ded@sihadc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani Ya eneo

Copyright ©2017 SihaDistrictCouncil . All rights reserved.