• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Serikali |
    • Malalamiko |
Siha District Council
Siha District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serekali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Siha

  • Mwanzo
  • Historia
    • Dhima na Dira
    • Wasifu wa Wilaya
  • Utawala
    • Muundo wa Kiutawala
    • Idara
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Kilimo,Ushirika na Umwagiliaji
      • Idara ya Mipango,Takwimu na Umwagiliaji
      • Idara ya Elimu Msingi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
    • Kata
      • Sanya Juu
      • Gararagua
      • Karansi
      • Biriri
      • Songu
      • Makiwaru
      • Olkolili
      • Ormelili
      • DonyoMuruak
      • Ngarenairobi
      • Ndumet
      • Mitimirefu
      • Livishi
      • Nasai
      • Kirua
      • Kashashi
      • Ivaeny
  • Huduma zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za maji
    • huduma za Watumishi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Tourism
  • Machapisho
    • Fomu za Maombi
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria
    • Jarida Mtandaoni Kila mwezi
  • Kituo cha habari
    • Maktaba ya Picha
    • Videos
    • Hutuba
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Elimu,Afya na Maji
      • Ujenzi,Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
      • Wajumbe Mkutano wa ALAT
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba vikao 2022/2023
    • Ratiba M/Kiti Halmashauri

Wananchi watakiwa kupinga ukatili wa Kijinsia:DC Siha

Posted on: September 8th, 2022

Mkuu wa Wilaya ya Siha mhe. Thomas Apson ametoa wito kwa jamii ya wananchi na wakazi wa Wilaya ya Siha mkoa wa Kilimanjaro kuweka mikakati ya pamoja ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto unaoendelea kwa miaka mingi sasa.

kauli hiyo ameitoa  leo 8 Septemba,2022 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha alipokuwa katika uzinduzi wa mpango wa mwaka mmoja wa shirika lisilo la Kiserikali NAFGEM walioanzisha mpango wa kuelimisha jamii jinsi ya kupinga na kuachana na mila potofu za ukatili dhidi ya watoto na wanawake hususani kuepukana na ukeketaji wa Wanawake.

"Napenda kuwaomba wananchi kuwa zipo mila ambazo zimepitwa na wakati ambazo kwa dunia ya leo tunatakiwa kuziacha kwani zinaleta madhara makubwa kwa jamii yetu ikiwemo suala la unyanyasaji wa kijinsia hususani wanawake na watoto" alisema Thomas Apson Mkuu wa Wilaya ya Siha

 

Akitoa taarifa ya mradi huo kwa kamati ya lishe Wilaya ya Siha ,mwakilishi wa shirika la NAFGEM ndugu Magdalena Lameck alisema kuwa shirika lisilo la Kiserikali NAFGEM limeweka malengo mahususi ya kuifikia jamii ya wananchi wa Wilaya ya Siha katika awamu tofautitofauti na kwa kuanzia mradi utaanza katika kata ya Karansi na utadumu kwa muda wa mwaka mmoja kuanzia mwezi Septemba,2022.

 

Ameeleza kuwa lengo la mradi huo ni kuelimisha jamii juu ya lishe bora na mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto hususani jamii kuachana na suala la ukeketaji kwa wanawake.

Pia aliwashukuru Viongozi wa Wilaya ya Siha kwa ushirikiano mkubwa wanaoendelea kutoa kwa shirika la NAFGEM katika mipango mbalimbali ya kuimarisha mtandao wa kuelimisha jamii juu ya madhara ya ukeketaji kwa wanawake na ameomba ushirikiano huo kuendelea zaidi ili kufikia malengo ya Serikali na jamii kwa ujumla.

"Napenda kuwahakikishia Kamati ya lishe na wananchi wa Siha kuwa NAFGEM itaendelea kuweka mpango wa kuzifikia kata nyingine 16  za Wilaya ya Siha zilizobaki bila kufikiwa katika mpango huu muhimu na  hii itategemea sana na upatikanaji wa bajeti kutoka shirika letu" alisema Magdalena.

Mwisho baada ya uzinduzi Mkuu wa Wilaya ya Siha mhe. Thomas Apson ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa mradi wa Lishe na Mapambano dhidi ya ukatili wa Kijinsia ametoa wito kwa mashirika mengine yasiyo ya Kiserikali kuiga mfano mzuri wa NAFGEM wa kuunga mkono juhudi za Serikali za kuimarisha lishe bora kwa jamii na mapambano dhidi ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.


Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA WALIOITWA KAZINI SIHA DC OKTOBA 2024 October 21, 2024
  • TANGAZO LA KOSEGEZWA MBELE UKODISHAJI WA MASHAMBA January 22, 2025
  • TANGAZO NAFASI YA MWENYEKITI BODI YA AJIRA HALMASHAURI YA SIHA KILIMANJARO February 18, 2025
  • TANGAZO NAFASI ZA KAZI SIHA August 28, 2020
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • Rais Samia aendelea kuitangaza Tanzania Kimataifa

    April 11, 2025
  • Rais Samia aendelea kuitangaza Tanzania Kimataifa

    April 11, 2025
  • Uzinduzi Sera ya Ardhi Siha yashiriki

    March 17, 2025
  • Umoja wa Ulaya kuendelea kushirikiana na Tanzania

    March 12, 2025
  • Ona Zote

Video

WATUMISHI SIHA DC WAASWA KUFANYA KAZI KWA UADILIFU
Video zingine

Viunganisho vya haraka

  • Wasifu wa Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Wasifu wa Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri
  • Soma taarifa zote ndani ya tovuti
  • Blog ya Halmashauri
  • facebook ya Halmashauri
  • Matokeo ya Taifa Darasa la Saba 2016 Siha
  • kuomba pasipoti kupitia mtandaoni
  • WARAKA WA MAVAZI KWA WATUMISHI WA UMMA
  • Fomu za Likizo Watumishi wa Umma

Viunganisho Vinavyohusiana

  • Basic Education Statistics
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Takwimu za taifa
  • Idara ya habari maelezo
  • tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Wananchi Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotazama

free HitCounter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji,Halmashauri ya Wilaya ya Siha /Siha District Council

    sanduku la Posta: 5 BR- Sanya Juu -Elerai S.L.P 129, 25482 SIHA

    simu: 0272-970677

    Mobile: 0713164432 DED Siha

    Email: ded@sihadc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani Ya eneo

Copyright ©2017 SihaDistrictCouncil . All rights reserved.