• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Serikali |
    • Malalamiko |
Siha District Council
Siha District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serekali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Siha

  • Mwanzo
  • Historia
    • Dhima na Dira
    • Wasifu wa Wilaya
  • Utawala
    • Muundo wa Kiutawala
    • Idara
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Kilimo,Ushirika na Umwagiliaji
      • Idara ya Mipango,Takwimu na Umwagiliaji
      • Idara ya Elimu Msingi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
    • Kata
      • Sanya Juu
      • Gararagua
      • Karansi
      • Biriri
      • Songu
      • Makiwaru
      • Olkolili
      • Ormelili
      • DonyoMuruak
      • Ngarenairobi
      • Ndumet
      • Mitimirefu
      • Livishi
      • Nasai
      • Kirua
      • Kashashi
      • Ivaeny
  • Huduma zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za maji
    • huduma za Watumishi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Tourism
  • Machapisho
    • Fomu za Maombi
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria
    • Jarida Mtandaoni Kila mwezi
  • Kituo cha habari
    • Maktaba ya Picha
    • Videos
    • Hutuba
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Elimu,Afya na Maji
      • Ujenzi,Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
      • Wajumbe Mkutano wa ALAT
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba vikao 2022/2023
    • Ratiba M/Kiti Halmashauri

Wahanga wa Wanyama pori wapewa kifuta jasho

Posted on: June 21st, 2017

Wananchi wawili wa Kijiji cha Mitimirefu kata ya Mitimirefu Tarafa ya Siha Magharibi wamepatiwa kifuta jasho kutoka Wizara ya Maliasili na utalii.

Tukio hilo limefanyika jana katika Kijiji cha Mitimirefu baada ya maofisa wa Maliasili kutoka ofisi ya kikosi cha kuzuia ujangili Kanda ya Kaskazini Arusha walipofika kijiji hapo.

Kifuta jasho hicho kimetokana na uharibifu wa mazao uliofanywa na wanyama pori katika mashamba ya wananchi yaliyopo katika kijiji cha Mitimirefu mwaka 2015 ambapo Wanyama hao waliharibu mashamba ya nyanya na maharagwe.

Wananchi waliopata kifuta jasho hicho walikidhi vigezo vyote vilivyowekwa na Wizara ya maliasili na Utalii ikiwa ni pamoja na shamba la mazao yaliyoharibiwa kuwa umbali wa zaidi ya nusu kilomita kutoka eneo la hifadhi, ukubwa wa eneo lililoharibiwa kuwa heka moja au zaidi.

Mmoja wa wanufaika hao ndugu Joel Nekisa kutoka kijiji cha Mitimirefu aliishukuru Serikali kwa kusikia kilio chao hasa kwa kuwalipa kwa wakati kifuta jasho hicho japo ni kidogo ukilinganisha na uharibifu uliotokea.

Alieleza kuwa yeye na mwenzake Daudi Ndetaulo wamelipwa kiasi cha shilingi laki moja kila mmoja kama kifuta jasho cha mazao yao yaliyoharibiwa na Wanyama pori mwishoni mwa mwaka 2015.

Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Siha ndugu Valerian Juwal aliishukuru Wizara ya Maliasili na utalii kwa kufanikisha jambo hilo mapema ambapo limewajengea imani wananchi wa Siha juu ya Serikali yao Sikivu kuhusu masuala mbalimbali ya wananchi.

Alieleza kuwa halmashauri ya Siha kupitia idara ya Ardhi na Maliasili itaendelea kuwasaidia wananchi katika kuwazuia wanyama pori wanaoendelea kuingia katika mashamba ya Wananchi ili kupunguza uharibifu mkubwa unaoweza kusababishwa na wanyama hao.

Napenda kutoa wito kwa wananchi wa vijiji vyote vinavyopakana na hifadhi kuhakikisha kuwa wanashirikiana na Serikali ya Wilaya katika kutoa taarifa pindi wanapoona wanyama pori wameingia katika maeneo yao alieleza Juwal.

Wakati huo huo Serikali imetoa kiasi cha shilingi milioni moja kama kifuta machozi kwa familia ya mtu mmoja aliyeuwawa na Tembo katika Kijiji cha Mitimirefu mwaka 2016.

Wilaya ya Siha imekuwa ikivamiwa na makundi makubwa ya wanyama pori kutoka hifadhi ya wanyama pori arusha na nchi jirani ya Kenya kupitia Wilaya za Londido na Rombo.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA WALIOITWA KAZINI SIHA DC OKTOBA 2024 October 21, 2024
  • TANGAZO LA KOSEGEZWA MBELE UKODISHAJI WA MASHAMBA January 22, 2025
  • TANGAZO NAFASI YA MWENYEKITI BODI YA AJIRA HALMASHAURI YA SIHA KILIMANJARO February 18, 2025
  • TANGAZO NAFASI ZA KAZI SIHA August 28, 2020
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • Rais Samia aendelea kuitangaza Tanzania Kimataifa

    April 11, 2025
  • Rais Samia aendelea kuitangaza Tanzania Kimataifa

    April 11, 2025
  • Uzinduzi Sera ya Ardhi Siha yashiriki

    March 17, 2025
  • Umoja wa Ulaya kuendelea kushirikiana na Tanzania

    March 12, 2025
  • Ona Zote

Video

WATUMISHI SIHA DC WAASWA KUFANYA KAZI KWA UADILIFU
Video zingine

Viunganisho vya haraka

  • Wasifu wa Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Wasifu wa Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri
  • Soma taarifa zote ndani ya tovuti
  • Blog ya Halmashauri
  • facebook ya Halmashauri
  • Matokeo ya Taifa Darasa la Saba 2016 Siha
  • kuomba pasipoti kupitia mtandaoni
  • WARAKA WA MAVAZI KWA WATUMISHI WA UMMA
  • Fomu za Likizo Watumishi wa Umma

Viunganisho Vinavyohusiana

  • Basic Education Statistics
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Takwimu za taifa
  • Idara ya habari maelezo
  • tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Wananchi Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotazama

free HitCounter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji,Halmashauri ya Wilaya ya Siha /Siha District Council

    sanduku la Posta: 5 BR- Sanya Juu -Elerai S.L.P 129, 25482 SIHA

    simu: 0272-970677

    Mobile: 0713164432 DED Siha

    Email: ded@sihadc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani Ya eneo

Copyright ©2017 SihaDistrictCouncil . All rights reserved.