• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Serikali |
    • Malalamiko |
Siha District Council
Siha District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serekali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Siha

  • Mwanzo
  • Historia
    • Dhima na Dira
    • Wasifu wa Wilaya
  • Utawala
    • Muundo wa Kiutawala
    • Idara
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Kilimo,Ushirika na Umwagiliaji
      • Idara ya Mipango,Takwimu na Umwagiliaji
      • Idara ya Elimu Msingi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
    • Kata
      • Sanya Juu
      • Gararagua
      • Karansi
      • Biriri
      • Songu
      • Makiwaru
      • Olkolili
      • Ormelili
      • DonyoMuruak
      • Ngarenairobi
      • Ndumet
      • Mitimirefu
      • Livishi
      • Nasai
      • Kirua
      • Kashashi
      • Ivaeny
  • Huduma zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za maji
    • huduma za Watumishi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Tourism
  • Machapisho
    • Fomu za Maombi
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria
    • Jarida Mtandaoni Kila mwezi
  • Kituo cha habari
    • Maktaba ya Picha
    • Videos
    • Hutuba
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Elimu,Afya na Maji
      • Ujenzi,Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
      • Wajumbe Mkutano wa ALAT
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba vikao 2022/2023
    • Ratiba M/Kiti Halmashauri

Vifaa Tiba Shilingi Milioni 80 vyapokelewa Hospitali ya Wilaya

Posted on: September 5th, 2023

 VIFAA TIBA SHILINGI MILIONI 80 VYAPOKEWA HOSPITAL YA WILAYA 

Naibu Waziri wa Afya na Mbunge wa Jimbo la Siha Mhe. Dkt Godwin Mollel amezishukuru Taasisi za Kimataifa ya Rotary 1918 Winndsor Canada na Taasisi ya PANETA baada ya kukabidhi Ultrasound na vifaa tiba vingine vyenye thamani ya zaidi ya Shilingi milioni 80 katika Hospitali ya Wilaya ya Siha.

Naibu Waziri Mhe Dkt. mollel amesema hayo Septemba 03, 2023 katika hafla ya kumkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Siha Mhe. Dkt Christopher Timbuka vifaa tiba hivyo,hafla  iliyofanyika kwenye Hospitali ya Wilaya ya Siha ambapo amesema lengo la kukabidhi vifaa tiba katika Hospitali hiyo ni kuongeza ufanisi na ubora wa huduma zinazotolewa kwa mama na mtoto.

Amesema Serikali imelipa kipaumbele eneo la afya ya mama na mtoto ili kuhakikisha vifo vya mama na mtoto nchini vinapungua au kumalizika kabisa.

“Tumekuwa tukiomba wadau na washirika wetu wa maendeleo watusaidie vifaa tiba katika maeneo mbalimbali  hapa nchini na kipaumbele kwenye eneo la afya ya mama na mtoto na Mhe. Rais wetu, anataka kupunguza/kumaliza  vifo vya mama na mtoto nchini” amesema Naibu Waziri Dkt Mollel

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Siha Mhe Dkt. Christopher Timbuka akipokea viaa hivyo ,amesema kuwa vifaa vilivyopokewa vitasaidia kurahisisha matibabu kwa wanawake zaidi ya 350 ndani ya Wilaya na wengine zaidi ya 80 kutoka nje ya Wilaya wanaohudumia kila mwezi katika Hospitali ya Wilaya ya Siha.

Amesema vifaa tiba hivyo vitatumika kwa lengo lililokusudiwa la kuwahudumia wananchi wanaofika kutibiwa katika Hospitali ya Wilaya hali itakayosaidia kupunguza gharama za kufuata huduma katika maeneo mengine nje ya Wilaya.

“Na sisi tutahakikisha kuwa tunavitunza ili viweze kuwahudumia watu wengi zaidi na watu waone manufaa ya vifaa hivi, na tunaishukuru sana Diplomasia ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa sababu ndiyo inayotufanya tunakubalika kwa watu katika maeneo mbalimbali duniani” ameongeza Mhe. Dkt Timbuka.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Taasisi ya Kimataifa ya Rotary 1918 Winndsor kutoka nchini Canada Daktari Mkunga Andrea Cassidy amesema lengo la kutoa vifaa hivyo ni kuhakikisha huduma bora na salama kwa mama na mtoto inapatikana bila kujali eneo alilopo mwananchi na wataendeleo kutoa mafunzo ya namna ya kutumia vifaa hivyo kwa Wataalamu wa Afya katika Hospitali ya Wilaya ya Siha.

Hospitali ya Wilaya ya Siha imepokea “Ultrasound” na vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya Milioni 80 kutoka taasisi ya Kimataifa ya Rotary 1918 Winndsor Canada na Taasisi ya PANETA kwa uratibu uliofanywa na Serikali kupitia Wizara ya Afya ili kuboresha zaidi huduma za mama na mtoto katika Hospitali hiyo.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA WALIOITWA KAZINI SIHA DC OKTOBA 2024 October 21, 2024
  • TANGAZO LA KOSEGEZWA MBELE UKODISHAJI WA MASHAMBA January 22, 2025
  • TANGAZO NAFASI YA MWENYEKITI BODI YA AJIRA HALMASHAURI YA SIHA KILIMANJARO February 18, 2025
  • TANGAZO NAFASI ZA KAZI SIHA August 28, 2020
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • Rais Samia aendelea kuitangaza Tanzania Kimataifa

    April 11, 2025
  • Rais Samia aendelea kuitangaza Tanzania Kimataifa

    April 11, 2025
  • Uzinduzi Sera ya Ardhi Siha yashiriki

    March 17, 2025
  • Umoja wa Ulaya kuendelea kushirikiana na Tanzania

    March 12, 2025
  • Ona Zote

Video

WATUMISHI SIHA DC WAASWA KUFANYA KAZI KWA UADILIFU
Video zingine

Viunganisho vya haraka

  • Wasifu wa Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Wasifu wa Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri
  • Soma taarifa zote ndani ya tovuti
  • Blog ya Halmashauri
  • facebook ya Halmashauri
  • Matokeo ya Taifa Darasa la Saba 2016 Siha
  • kuomba pasipoti kupitia mtandaoni
  • WARAKA WA MAVAZI KWA WATUMISHI WA UMMA
  • Fomu za Likizo Watumishi wa Umma

Viunganisho Vinavyohusiana

  • Basic Education Statistics
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Takwimu za taifa
  • Idara ya habari maelezo
  • tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Wananchi Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotazama

free HitCounter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji,Halmashauri ya Wilaya ya Siha /Siha District Council

    sanduku la Posta: 5 BR- Sanya Juu -Elerai S.L.P 129, 25482 SIHA

    simu: 0272-970677

    Mobile: 0713164432 DED Siha

    Email: ded@sihadc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani Ya eneo

Copyright ©2017 SihaDistrictCouncil . All rights reserved.