• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Serikali |
    • Malalamiko |
Siha District Council
Siha District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serekali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Siha

  • Mwanzo
  • Historia
    • Dhima na Dira
    • Wasifu wa Wilaya
  • Utawala
    • Muundo wa Kiutawala
    • Idara
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Kilimo,Ushirika na Umwagiliaji
      • Idara ya Mipango,Takwimu na Umwagiliaji
      • Idara ya Elimu Msingi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
    • Kata
      • Sanya Juu
      • Gararagua
      • Karansi
      • Biriri
      • Songu
      • Makiwaru
      • Olkolili
      • Ormelili
      • DonyoMuruak
      • Ngarenairobi
      • Ndumet
      • Mitimirefu
      • Livishi
      • Nasai
      • Kirua
      • Kashashi
      • Ivaeny
  • Huduma zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za maji
    • huduma za Watumishi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Tourism
  • Machapisho
    • Fomu za Maombi
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria
    • Jarida Mtandaoni Kila mwezi
  • Kituo cha habari
    • Maktaba ya Picha
    • Videos
    • Hutuba
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Elimu,Afya na Maji
      • Ujenzi,Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
      • Wajumbe Mkutano wa ALAT
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba vikao 2022/2023
    • Ratiba M/Kiti Halmashauri

TAARIFA MWENYEKITI WA HALMASHAURI KWA UMMA TAREHE 21.04.2021

Posted on: April 21st, 2021

OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA


HALMASHAURI YA WILAYA YA SIHA

TAARIFA YA MWENYEKITI WA HALMASHAURI MKUTANO WA KAWAIDA WA  BARAZA LA MADIWANI  TAREHE 21/04/2021  KATIKA KIPINDI CHA ROBO YA TATU   MWAKA WA FEDHA 2020/2021.

Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Siha,

Mwakilishi Ofisi ya RAS-Mkoa wa Kilimanjaro,

Mh. Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Siha,

Mhe. Makamu Mwenyekiti Halmashhauri ya Siha

Waheshimiwa Madiwani,

Ndugu Mkurugenzi  Mtendaji Halmashauri ya Siha (Katibu wa Baraza),

Wah Viongozi wa Madhehebu ya  Dini,

Wageni Waalikwa,

Ndugu Wataalamu,

Waandishi wa Habari,

Wananchi wa Wilaya ya Siha,

Mabibi na Mabwana,

Nawasalimu wote kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ……. Kazi inaendelea, Napenda kumshukuru Mungu kwa ajili wema na Baraka na kutuweka salama na kutupa nguvu za kuwatumikia Wananchi na Wakazi wa Siha.  Kwa niaba ya Baraza la Wah. Madiwani napenda kutoa shukrani za dhati kwa Viongozi mbalimbali wa madhehebu ya Dini kwa jinsi wanavyoendelea kuiombea Wilaya yetu ili  izidi kuwa na maendeleo pamoja na kudumisha amani miongoni mwetu. Nafurahi pia kuona watumishi wa Umma katika Wilaya yetu wakiendelea kutoa ushirikiano wa kutosha kwa ajili ya kutoa huduma mbalimbali kwa jamii yetu.Naomba tena upendo na umoja wetu uzidi kuendelea wakati wote kwani palipo na umoja na upendo basi mafanikio yatakuwepo.

Vilevile napenda kuwashukuru Wananchi wa Kata ya Karansi kwa jinsi wanavyoendelea kuniamini na kunipa ushirikiano katika wajibu wangu wa kuwatumikia pamoja na jukumu la Mwenyekiti wa Halmashauri ambapo sasa natakiwa kuwatumikia Wananchi wote wa Halmashauri ya Siha.

 

Wah. Madiwani ,  na Ndugu  Wananchi,

Katika taarifa yangu hii fupi yapo mambo machache ambayo nimeona niyazungumzie kama sehemu ya muendelezo wa taarifa zangu ili kwa namna moja au nyingine itasaidia kujua muelekeo  na dira ya maendeleo katika Halmashauri yetu.

UKUSANYAJI WA MAPATO

Waheshimiwa Madiwani, Ndugu Wananchi

Katika suala la  ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri,  napenda kuendelea kutoa wito kwa Wataalam kufuatilia kwa karibu zoezi la ukusanyaji wa mapato pamoja na kubuni vyanzo vipya vya mapato ya Halmashauri kwa kushirikiana na Waheshimiwa madiwani. Dunia imebadilika hivyo ni budi na sisi kubadilika ili kuendana na wakati hususani kubuni miradi mikubwa na ya kudumu badala ya kuendelea kusubiri ushuru wa mazao pamoja na viwanja kama vyanzo vikuu vya  mapato ya Halmashauri.

Naomba kutoa wito kwa Mkurugenzi Mtendaji na Wataalam wa Halmashauri kuhakikisha kuwa hadi mwisho wa mwaka huu wa fedha 2020/2021 ukusanyaji wa mapato ufikie malengo ya zaidi ya asilimia 80 kama ilivyo agizo Serikali yetu tukufu.

Wah. Madiwani ,  na Ndugu  Wananchi

Ili kufanikisha zoezi hili la  ukusanyaji wa mapato naomba kila Mhe. Diwani katika Kata yake atusaidie kubuni na kutoa taarifa ya vyanzo/chanzo kipya cha mapato ili kiwezeshe  katika kuboresha utoaji wa huduma muhimu kwa Wananchi katika Halmashauri yetu. Aidha, nawasihi na kuwaomba waheshimiwa Madiwani kutoa taarifa kwa Mkurugenzi Mtendaji pale wanapoona kuna hujuma za ukwepaji na ulipaji wa mapato ya Serikali na Halmashauri yetu ili hatua za haraka ziweze kuchukuliwa na mamlaka zinazohusika. Naomba kutoa wito kwa Mkurugenzi Mtendaji kuweka jitihada zaidi katika usimamizi wa mapato katika Stendi ya KIA, hapa bado naona mapato bado hayajakusanywa kwa asilimia mia kwani bado kuna magari ambayo hayaingii stendi. Naomba juhudi ziendelee za kuyafanya magari yote yaingie stendi ili mapato yaongezeke

 

 

SEKTA YA  KILIMO NA MIFUGO

Wah. Madiwani na Ndugu Wananchi

 Napenda kuwashukuru wananchi na wakazi wa Wilaya ya Siha kwa jinsi wanavyoendelea kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya Sita katika shughuli za kilimo na mifugo hapa Wilayani Siha. Kipekee namshukuru Mungu kwa Baraka za mvua za masika zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya Wilaya yetu japo mvua za mwaka huu zimeonekana kuchelewa kidogo ukilinganisha na miaka mingine ya hivi karibuni,naomba Wananchi wetu tuendelee kufuatilia taarifa za mamlaka ya hali ya hewa pamoja na wataalam wa kilimo waliopo katika Vijiji vyetu ili kuwa na kilimo chenye tija.

Katika kipindi cha robo ya tatu kama mlivyosikia na kuona katika vyombo vya Habari hapa Nchini Wilaya yetu ilivamiwa na kundi la nzige ambao walikuwepo katika Tarafa ya Siha Magharibi na wengine wachache katika maeneo mengine ya Wilaya yetu.Napenda kuishukuru Serikali yetu ya Tanzania kupitia Wizara ya Kilimo ilivyoweza kupambana na nzige hao na hatimaye walimalizika kabisa katika maeneo yetu ya Wilaya ya Siha. Vilevile kwa niaba ya Baraza la Madiwani napenda kutoa shukrani za dhati kwa Kamati ya ulinzi na usalama katika Wilaya yetu ikiongozwa na Mkuu wetu wa Wilaya ya Siha Mheshimiwa Onesmo Buswelu kwa jinsi walivyoshiriki kikamilifu katika zoezi la kupambana na nzige,kwani walifanya kazi hii usiku na mchana bila hata kupumzika.

Wah. Madiwani , na Ndugu  Wananchi

Katika kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara katika Halmashauri yetu naomba kutoa wito kwa Wataalam wa Kilimo waliopo katika Kata na Vijiji vyetu waendelee kutumia utaalam wao vizuri ili uwasaidie wananchi katika uzalishaji na nashauri Wataalam wetu wa kilimo  waondokana na tabia ya kufanya kazi kwa mazoea.

Katika kuboresha sekta ya Kilimo naomba Halmashauri yetu kupitia Wizara ya Kilimo ione namna ya kuboresha miundombinu ya umwagiliaji kwa kuboresha  mifereji na Mabwawa ya umwagiliaji ili kuwa na Kilimo cha kisasa na cha uhakika.

Kwa upande wa Wataalam wa mifugo naomba pia wataalamu hawa waendelee kutoa utaalamu wao ili kusaidia uzalishaji wa mifugo bora na ya kisasa ili kuwaongezea kipato wananchi wetu  wa Wilaya ya Siha. Napenda kukupongeza Mkurugenzi kwa jinsi unavyoendelea kuchukua hatua za kuhakikisha kuwa wataalam hawa wa mifugo wanafanya kazi walizopangiwa kulingana na ajira zao. Naomba nitoe wito kwa watumishi hawa maofisa Ugani kuwa wanatakiwa  kuendelea kutumia utaalamu wao ili kuwanufaisha wananchi wetu na jamii ya WanaSiha kwa ujumla wake

UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO

Wah. Madiwani na Ndugu Wananchi

Katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri yetu ya Wilaya ya Siha, naomba kutoa shukrani za pekee kwa Serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kutuamini na  kutupatia fedha nyingi za kutekeleza miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Siha. Halmashauri ya Siha katika kipindi cha robo ya tatu tumepokea shilingi Milioni 650 za kukamilisha jengo la makao makuu ya Halmashauri yetu kazi imeanza na inaendelea kama wengine wengi mlivyoona,Halmashauri yetu imepokea pia shilingi Milioni 210 kutoka Serikali kuu kwa ajili ya kukamilisha  Maabara 7 za shule za Sekondari shule hizo ni Oshara,Fuka,Jitegemee,Dahani,Esinyari,Magadini,Karansi  ambapo kila shule imepata shilingi Milioni 30, Pia Serikali yetu imetupatia shilingi Milioni 150 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Zahanati Tatu za Mese,Roseline na Sinai ambapo kati  ya fedha hizo  kila Zahanati imepatiwa shilingi milioni 50 na kazi zinaendelea vizuri katika maeneo yote ya miradi. Katika miradi ya elimu msingi Serikali imetoa shilingi Milioni 125 za kukamilisha maboma katika ujenzi wa darasa moja katika shule kumi za msingi.Hii ni Hatua kubwa iliyofanywa na Serikali yetu Tukufu chini ya Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan.

Aidha, katika kipindi hiki cha robo ya tatu Halmashauri yetu imepokea pia shilingi milioni 500 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya ujenzi katika Hospital yetu ya Wilaya na nimeambiwa kuwa ujenzi wa wodi mbili ya Wanaume na Wanawake umeshaanza kufanyika. Naomba kutoa wito kwa Watumishi na Wataalam wa Halmashauri hususani CMT kuhakikisha kuwa wanamsaidia Mkurugenzi Mtendaji katika kusimamia kazi za ujenzi kufanyika katika viwango vya juu kama ilivyo katika mradi wa ujenzi uliofanyika katika  shule ya Sekondari Namwai.Mimi kama Mwenyekiti wa Halmashauri ya Siha pamoja na Baraza langu hatutakubali wala kuvumilia uzembe wala utendaji kazi usioridhisha katika usimamizi wa fedha za umma,naomba kila mtu atimize wajibu wake.

Waheshimiwa  Madiwani na ndg Wananchi;

Kabla ya kufika mwisho wa Taarifa yangu, napenda tena Kumshukuru Mungu kwa jinsi anavyoendelea kuibariki Nchi yetu kuwa na amani na utulivu hasa baada ya Nchi yetu kupitia kipindi cha maumivu cha kumpoteza Jemedari wetu na mzalendo namba moja na shujaa wa Afrika Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Naomba sisi sote tuendelee kumwombea rais wetu wa awamu ya Sita Mhe. Samia Suluhu Hassan ili Mungu ampe nguvu na maono ya kuongoza Nchi yetu kwa ustawi wa maendeleo ya Wananchi na Nchi yetu izidi kupata mafanikio katika Nyanja za kiuchumi,kiutamaduni, Kisiasa na Kijamii.

Vilevile napenda kutoa wito kwa Wah.Madiwani ,Watumishi na Wananchi wa Siha tuzidi kupendana na kushikamana zaidi ili kufikia malengo ya maendeleo na kuboresha maisha ya wananchi wetu kwa kushirikiana na Serikali yetu tukufu inayosimamiwa na Chama cha Mapinduzi. Waswahili wanasema umoja ni nguvu na utengano ni ughaifu. JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA………………………………………………………….

Mwisho kabisa,nichukue fursa hii  kuwashukuru Wah. Madiwani kwa kuhudhuria na  usikivu  wenu mzuri tangu mwanzo wa taarifa yangu hadi sasa ,Pia wataalam wa Halmashauri nawashukuru kwa maandalizi mazuri ya mkutano huu wa Baraza la Wah. Madiwani ambao umekuwepo hapa tangu jana hadi leo. Napenda kuwashukuru tena Wananchi na Wakazi wa Siha kwa jinsi mnavyotoa ushirikiano kwa Halmashauri yetu hususani katika kulipa ushuru mbalimbali kwa mujibu wa sheria ambao umewezesha Halmashauri kuboresha utoaji wa huduma kwa jamii yetu hasa utekelezaji wa miradi ya maendeleo. naomba usikivu na utulivu huu uendelee hadi mwisho wa Mkutano wetu na hatimaye tumalize na kuagana kwa upendo, furaha na amani.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA……….

Asanteni  sana kwa kunisikiliza

Imetolewa na:

 

Mhe. Duncan B. Urassa

Mwenyekiti wa Halmashauri (W)

SIHA

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA WALIOITWA KAZINI SIHA DC OKTOBA 2024 October 21, 2024
  • TANGAZO LA KOSEGEZWA MBELE UKODISHAJI WA MASHAMBA January 22, 2025
  • TANGAZO NAFASI YA MWENYEKITI BODI YA AJIRA HALMASHAURI YA SIHA KILIMANJARO February 18, 2025
  • TANGAZO NAFASI ZA KAZI SIHA August 28, 2020
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • Rais Samia aendelea kuitangaza Tanzania Kimataifa

    April 11, 2025
  • Rais Samia aendelea kuitangaza Tanzania Kimataifa

    April 11, 2025
  • Uzinduzi Sera ya Ardhi Siha yashiriki

    March 17, 2025
  • Umoja wa Ulaya kuendelea kushirikiana na Tanzania

    March 12, 2025
  • Ona Zote

Video

WATUMISHI SIHA DC WAASWA KUFANYA KAZI KWA UADILIFU
Video zingine

Viunganisho vya haraka

  • Wasifu wa Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Wasifu wa Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri
  • Soma taarifa zote ndani ya tovuti
  • Blog ya Halmashauri
  • facebook ya Halmashauri
  • Matokeo ya Taifa Darasa la Saba 2016 Siha
  • kuomba pasipoti kupitia mtandaoni
  • WARAKA WA MAVAZI KWA WATUMISHI WA UMMA
  • Fomu za Likizo Watumishi wa Umma

Viunganisho Vinavyohusiana

  • Basic Education Statistics
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Takwimu za taifa
  • Idara ya habari maelezo
  • tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Wananchi Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotazama

free HitCounter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji,Halmashauri ya Wilaya ya Siha /Siha District Council

    sanduku la Posta: 5 BR- Sanya Juu -Elerai S.L.P 129, 25482 SIHA

    simu: 0272-970677

    Mobile: 0713164432 DED Siha

    Email: ded@sihadc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani Ya eneo

Copyright ©2017 SihaDistrictCouncil . All rights reserved.