• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Serikali |
    • Malalamiko |
Siha District Council
Siha District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serekali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Siha

  • Mwanzo
  • Historia
    • Dhima na Dira
    • Wasifu wa Wilaya
  • Utawala
    • Muundo wa Kiutawala
    • Idara
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Kilimo,Ushirika na Umwagiliaji
      • Idara ya Mipango,Takwimu na Umwagiliaji
      • Idara ya Elimu Msingi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
    • Kata
      • Sanya Juu
      • Gararagua
      • Karansi
      • Biriri
      • Songu
      • Makiwaru
      • Olkolili
      • Ormelili
      • DonyoMuruak
      • Ngarenairobi
      • Ndumet
      • Mitimirefu
      • Livishi
      • Nasai
      • Kirua
      • Kashashi
      • Ivaeny
  • Huduma zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za maji
    • huduma za Watumishi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Tourism
  • Machapisho
    • Fomu za Maombi
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria
    • Jarida Mtandaoni Kila mwezi
  • Kituo cha habari
    • Maktaba ya Picha
    • Videos
    • Hutuba
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Elimu,Afya na Maji
      • Ujenzi,Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
      • Wajumbe Mkutano wa ALAT
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba vikao 2022/2023
    • Ratiba M/Kiti Halmashauri

Mafunzo kazini kwa Walimu 210 yafunguliwa Wilayani Siha

Posted on: March 13th, 2023

MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU 210 SHULE ZA SEKONDARI SIHA DC KILIMANJARO


13 Machi,2023


Halmashauri ya Wilaya ya Siha Mkoa wa Kilimanjaro imeandaa mafunzo ya Siku 4 Kazini kwa Walimu wa Shule zote za  Sekondari za Serikali Wilaya ya Siha.

Mafunzo haya  kwa Walimu kazini yamefunguliwa leo *tarehe 13.3.2023* na Dkt.Barnabas Mbwambo  Kaimu  Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Siha kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji.

Awali kabla ya ufunguzi wa Mafunzo Mkuu wa Divisheni ya Elimu Sekondari Mwalimu Naomi Swai alisema kuwa, mafunzo kwa Walimu kazini yanafanyika kuanzia tarehe 13/03/2023 Hadi tarehe 16/03/2023.

 Kundi la kwanza la  Walimu wa Sayansi ya Jamii linaanza leo tarehe 13/3/2023 hapa Kilingi Sekondari na litamaliza kesho tarehe 14.03.2022 na kundi la pili ni Walimu wa Sayansi na Hisabati ambapo mafunzo yatafanyika tarehe 15 na 16/3/2023 katika shule ya Sekondari Sanya Juu alisema Naomi Swai.

"Maudhui ya mafunzo haya ni pamoja na utekelezaji wa Mtaala wa Ujenzi wa ujuzi(competence based Curriculum),mbinu bainifu za kufundishia,matumizi fanisi ya zana za kufundishia,upimaji wa ufundishaji pamoja na matumizi fanisi ya Tekinolojia katika ufundishaji na ujifunzaji" alisema na kuongeza.

Mwalimu Naomi Swai  pia alisema  kuwa, mafunzo haya yameandaliwa kuleta tija kwa kuwa Kila Mwalimu anahusika moja kwa moja kupata mbinu za kuboresha ufundishaji Kwa matokeo chanya ya ujenzi wa ujuzi.

Akifungua mafunzo hayo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Dkt.Barnabas Mbwambo amesema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya  Siha inamategemeo makubwa na mafunzo haya kuleta Mabadiliko chanya katika sekta ya elimu Sekondari Wilayani Siha hususani kuongeza ufaulu wa Wanafunzi katika Masomo mbalimbali.


"Napenda niwape angalize kuwa,Ubora wa Mafunzo mtakayopata hapa utatokana na utayari wenu kuona kuwa hii ni fursa muhimu itakayoleta Mabadiliko katika ufundishaji na ujifunzaji wa Masomo mnayofundisha" alisema Dkt.Barnabas Mbwambo.

Pia alisema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Siha itaendelea kuhakikisha kuwa Walimu wa Shule za Sekondari na Msingi wanapata msaada unaohitajika ili waweze kutekeleza Majukumu yao ya kuelimisha Jamii na Taifa kwa ujumla.


Kabla ya kuhitinisha hotuba yake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji aliwaambia Washiriki wa Mafunzo hayo kuwa,Taifa linawategemea sana Walimu katika maboresho ya elimu ambapo pia Walimu wanalo jukumu kubwa la kulinda Maadili,kujenga uzalendo pamoja na kuandaa raia wema na wenye uwezo wa kuleta maendeleo endelevu ya Taifa.


Wilaya ya Siha inajumla ya Shule 21 za Sekondari Kati ya hizo shule 15 zinamilikiwa na Serikali na shule 6 zinamilikiwa na Mashirika ya Dini na Watu binafsi.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA WALIOITWA KAZINI SIHA DC OKTOBA 2024 October 21, 2024
  • TANGAZO LA KOSEGEZWA MBELE UKODISHAJI WA MASHAMBA January 22, 2025
  • TANGAZO NAFASI YA MWENYEKITI BODI YA AJIRA HALMASHAURI YA SIHA KILIMANJARO February 18, 2025
  • TANGAZO NAFASI ZA KAZI SIHA August 28, 2020
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • Rais Samia aendelea kuitangaza Tanzania Kimataifa

    April 11, 2025
  • Rais Samia aendelea kuitangaza Tanzania Kimataifa

    April 11, 2025
  • Uzinduzi Sera ya Ardhi Siha yashiriki

    March 17, 2025
  • Umoja wa Ulaya kuendelea kushirikiana na Tanzania

    March 12, 2025
  • Ona Zote

Video

WATUMISHI SIHA DC WAASWA KUFANYA KAZI KWA UADILIFU
Video zingine

Viunganisho vya haraka

  • Wasifu wa Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Wasifu wa Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri
  • Soma taarifa zote ndani ya tovuti
  • Blog ya Halmashauri
  • facebook ya Halmashauri
  • Matokeo ya Taifa Darasa la Saba 2016 Siha
  • kuomba pasipoti kupitia mtandaoni
  • WARAKA WA MAVAZI KWA WATUMISHI WA UMMA
  • Fomu za Likizo Watumishi wa Umma

Viunganisho Vinavyohusiana

  • Basic Education Statistics
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Takwimu za taifa
  • Idara ya habari maelezo
  • tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Wananchi Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotazama

free HitCounter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji,Halmashauri ya Wilaya ya Siha /Siha District Council

    sanduku la Posta: 5 BR- Sanya Juu -Elerai S.L.P 129, 25482 SIHA

    simu: 0272-970677

    Mobile: 0713164432 DED Siha

    Email: ded@sihadc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani Ya eneo

Copyright ©2017 SihaDistrictCouncil . All rights reserved.