• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Serikali |
    • Malalamiko |
Siha District Council
Siha District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serekali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Siha

  • Mwanzo
  • Historia
    • Dhima na Dira
    • Wasifu wa Wilaya
  • Utawala
    • Muundo wa Kiutawala
    • Idara
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Kilimo,Ushirika na Umwagiliaji
      • Idara ya Mipango,Takwimu na Umwagiliaji
      • Idara ya Elimu Msingi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
    • Kata
      • Sanya Juu
      • Gararagua
      • Karansi
      • Biriri
      • Songu
      • Makiwaru
      • Olkolili
      • Ormelili
      • DonyoMuruak
      • Ngarenairobi
      • Ndumet
      • Mitimirefu
      • Livishi
      • Nasai
      • Kirua
      • Kashashi
      • Ivaeny
  • Huduma zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za maji
    • huduma za Watumishi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Tourism
  • Machapisho
    • Fomu za Maombi
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria
    • Jarida Mtandaoni Kila mwezi
  • Kituo cha habari
    • Maktaba ya Picha
    • Videos
    • Hutuba
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Elimu,Afya na Maji
      • Ujenzi,Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
      • Wajumbe Mkutano wa ALAT
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba vikao 2022/2023
    • Ratiba M/Kiti Halmashauri

HRT SACCOS YAZIDI KUNG’ARA YARUDISHA KWA JAMII

Posted on: July 22nd, 2025

Chama cha Akiba na Mikopo Hai Rural Teachers Saccos (HRT) kimekabidhi madawati 40 yenye thamani ya kiasi cha shilingi milioni nne katika shule ya Ngaremji iliyopo wilayani Siha Mkoani Kilimanjaro.

HRT Saccos imekabidhi madawati hayo Julai 22, 2025 ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa  msingi wa saba wa vyama vya ushirika unaohimiza   kurudisha kwa jamii faida inayopatikana ndani ya chama.

Akizungumza wakati wa kupokea madawati hayo mwakilishi wa mkuu wa wilaya ya Siha Shedrack Moshi ameishukuru HRT SACCOS kwa jitihada walizofanya na kuona umuhimu wa kurudisha kwa jamii na kwamba madawati hayo yanakwenda kuondoa msongamano wa wanafunzi darasani na kufanya ufaulu kuongezeka

 “Ndugu zangu nipende kusema kwa niaba ya serikali kwamba tumefarijika sana na jitihada hizi ambazo zimefanywa na chama hiki ambacho kimeona umuhimu wa kurudisha kwa jamii,na leo hii wamekabidhi madawati 40 kwa ajili ya watoto wetu katika shule hii,badala ya watoto kukaa kwa kusongamana sasa hivi wataweza kukaa vizuri na hivyo ule usikivu na kama alivyohaidi mwalimu mkuu ufaulu unaenda kuongezeka” Amesema Moshi

Awali akisoma taarifa ya HRT SACCOS  Mwalimu Alex Warioba ambae ni mwenyekiti wa chama hicho amesema kila mwaka chama kinatekeleza msingi wa saba wa vyama vya ushirika kwa kuendelea kuijali jamii na kwa mwaka 2025 wameona ni vyema kutoa madawati hayo ili  kupunguza upungufu wa madawati uliopo katika shule hiyo.

 “Mh mkuu wa wilaya kila mwaka chama kinatekeleza msingi wa saba wa ushirika kwa kuendelea kuijali jamii,na mwaka huu Mh mkuu wa wilaya tumetembelea shule hii ya  msingi Ngare Mji na tunatoa ambayo thamani yake ni shilingi milioni 4 ,mwaka huu chama kinaadhimisha miaka 25 tangu kuanzishwa”Amesema Mwalimu Warioba.

Nae afisa elimu msingi wilaya ya Siha Fatu Msangi amesema kupitia msaada huo wa madawati yaliyotolewa na HRT SACCOS yatafanya utekeleza wa mtaala kufanyika kwa ufanisi zaidi.

 “Thamani hizi mlizotupatia zitatufanya utekelezaji wa mtaala kufanyika kwa ufanisi zaidi kuliko ambavyo watoto wangekuwa wamesongamana hivyo tunawashukuru sana HRT SACCOS”Amesema Msangi

Kwa upande wao wanafunzi wa shule ya msingi Ngare Mji Sofia Yusuph na Asia Hussen wameishukuru HRT SACCOS na kuhaidi kutunza madawati hayo pamoja na kusoma kwa bidii.

Katika wiki ya maadhimisho ya miaka 25 ya HRT SACCOS imeendesha shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo michezo ya bonanza, kutoa elimu kwa jamii kupitia vyombo vya habari, na sasa kukabidhi madawati hayo kama sehemu ya mchango wake kwa maendeleo ya elimu nchini.

Matangazo

  • TANGAZO UTOAJI WA CHANJO HOMA YA MAPAFU NA UTAMBUZI WA NG'OMBE KWA HERENI WILAYA YA SIHA September 10, 2025
  • TANGAZO KWA UMMA MAPOKEZI YA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELEO SIHA DC KILIMANJARO SEPT.2025 September 16, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA MAPOKEZI YA FEDHA UTEKELEZAJI MIRADI YA MAENDELEO ROBO YA KWANZA 2025/2026 September 15, 2025
  • TANGAZO NAFASI ZA KAZI SIHA August 28, 2020
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • KAMATI YA MTAKUWWA SIHA WAPATIWA MAFUNZO KUKOMESHA UKATILI

    October 02, 2025
  • Maadhimisho siku ya Usafi Mazingira,Wananchi wajitokeza kwa wingi

    September 26, 2025
  • RC BABU AIPONGEZA SIHA DC KWA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA MASHULENI

    September 24, 2025
  • TEF YATOA BIMA ZA MISHA KWA VIKUNDI VYA MWITIKIO WA HARAKA SIHA

    September 22, 2025
  • Ona Zote

Video

MAOFISA MIFUGO SIHA WAPATIWA VITENDEA KAZI VYA KISASA
Video zingine

Viunganisho vya haraka

  • Wasifu wa Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Wasifu wa Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri
  • Soma taarifa zote ndani ya tovuti
  • Blog ya Halmashauri
  • facebook ya Halmashauri
  • Matokeo ya Taifa Darasa la Saba 2016 Siha
  • kuomba pasipoti kupitia mtandaoni
  • WARAKA WA MAVAZI KWA WATUMISHI WA UMMA
  • Fomu za Likizo Watumishi wa Umma

Viunganisho Vinavyohusiana

  • Basic Education Statistics
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Takwimu za taifa
  • Idara ya habari maelezo
  • tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Wananchi Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotazama

free HitCounter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji,Halmashauri ya Wilaya ya Siha /Siha District Council

    sanduku la Posta: 5 BR- Sanya Juu -Elerai S.L.P 129, 25482 SIHA

    simu: 0272-970677

    Mobile: 0713164432 DED Siha

    Email: ded@sihadc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani Ya eneo

Copyright ©2017 SihaDistrictCouncil . All rights reserved.