• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Serikali |
    • Malalamiko |
Siha District Council
Siha District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serekali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Siha

  • Mwanzo
  • Historia
    • Dhima na Dira
    • Wasifu wa Wilaya
  • Utawala
    • Muundo wa Kiutawala
    • Idara
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Kilimo,Ushirika na Umwagiliaji
      • Idara ya Mipango,Takwimu na Umwagiliaji
      • Idara ya Elimu Msingi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
    • Kata
      • Sanya Juu
      • Gararagua
      • Karansi
      • Biriri
      • Songu
      • Makiwaru
      • Olkolili
      • Ormelili
      • DonyoMuruak
      • Ngarenairobi
      • Ndumet
      • Mitimirefu
      • Livishi
      • Nasai
      • Kirua
      • Kashashi
      • Ivaeny
  • Huduma zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za maji
    • huduma za Watumishi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Tourism
  • Machapisho
    • Fomu za Maombi
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria
    • Jarida Mtandaoni Kila mwezi
  • Kituo cha habari
    • Maktaba ya Picha
    • Videos
    • Hutuba
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Elimu,Afya na Maji
      • Ujenzi,Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
      • Wajumbe Mkutano wa ALAT
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba vikao 2022/2023
    • Ratiba M/Kiti Halmashauri

Bei ya Maji Wilayani Siha-Kilimanjaro yaendelea kushuka

Posted on: August 15th, 2022

Bei ya Maji Wilaya ya Siha Mkoani Kilimanjaro  yaendelea kushuka

Wananchi Wilayani Siha waendelea kunufaika na kushuka kwa bei ya maji iliyotolewa na Wizara ya Maji hivi karibuni.

Akitoa taarifa katika Mkutano wa Baraza la Wah. Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha Mkoa wa Kilimanjaro uliofanyika hivi karibuni, Meneja wa RUWASA Wilaya ya Siha Mhandisi Emmy George amesema kuwa Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya Maji imetoa bei elekezi ya Maji kwa matumizi ya Majumbani,katika Taasisi na maeneo ya Biashara na Viwanda.

Meneja wa RUWASA SIHA Mhandisi Emmy George akitoa taarifa ya bei mpya za maji katika Baraza la Madiwani H/W Siha

Ameeleza kuwa bei elekezi ya matumizi ya maji majumbani kwa uniti moja itakuwa shilingi 700 tu kwa idadi yoyote ya kipimo mtumiaji atakachotumia,ambapo ni tofauti na hapo awali ilikuwa zaidi ya shilingi 850 kwa uniti moja ya maji(hakuna tena progressive).


Meneja wa RUWASA SIHA amewaambia wajumbe wa Baraza la Madiwani Halmashauri ya Siha kuwa,bei elekezi ya Maji kwa matumizi ya Biashara na Viwandani pia itabadilika kutoka shilingi 1200 na kushuka hadi  shilingi 1000 kwa uniti moja na hakuna pia progressive katika eneo hili.

Wah. Madiwani Halmashauri ya Siha wakisiliza taarifa ya maji kutoka meneja wa RUWASA SIHA

Katika maeneo ya Taasisi( kama vile Mashule,Vituo vya Afya,Zahanati,Hospitali), Meneja wa RUWASA Wilaya ya Siha alisema kuwa bei mpya  elekezi  ya maji itakuwa shilingi 700 tu kwa uniti moja ambapo pia hakuna kuongezeka kwa bei kulingana na matumizi ya Taasisi.

Wajumbe wa Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Siha wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa Siha

Katika Taarifa yake Meneja wa RUWASA Wilaya ya Siha amesema kuwa bei hizi mpya za maji zitaanza kutumika katika mwaka huu mpya wa fedha 2022/2023 hivyo wananchi wategemee kupata unafuu mkubwa kutokana na bei hizi.

Wilaya ya Siha ni Miongoni mwa Halmashauri za Mkoa wa Kilimanjaro zilizopata mafanikio makubwa katika usambazaji wa maji katika maeneo ya vijiji vyote 60 ,Kata 17 na Tarafa 5 na upatikanaji wa maji umefikia zaidi ya asilimia 85 kwa mwaka 2021/2022.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA WALIOITWA KAZINI SIHA DC OKTOBA 2024 October 21, 2024
  • TANGAZO LA KOSEGEZWA MBELE UKODISHAJI WA MASHAMBA January 22, 2025
  • TANGAZO NAFASI YA MWENYEKITI BODI YA AJIRA HALMASHAURI YA SIHA KILIMANJARO February 18, 2025
  • TANGAZO NAFASI ZA KAZI SIHA August 28, 2020
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • MILIONI 316.5 YATOLEWA KWA VIKUNDI 48 WILAYANI SIHA

    May 23, 2025
  • Mchengerwa awapongeza Maofisa Habari Nchini Kwa uchapa kazi

    May 23, 2025
  • Mchengerwa awapongeza Maofisa Habari Nchini Kwa uchapa kazi

    May 23, 2025
  • Mchengerwa awapongeza Maofisa Habari Nchini Kwa uchapa kazi

    May 23, 2025
  • Ona Zote

Video

WATUMISHI SIHA DC WAASWA KUFANYA KAZI KWA UADILIFU
Video zingine

Viunganisho vya haraka

  • Wasifu wa Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Wasifu wa Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri
  • Soma taarifa zote ndani ya tovuti
  • Blog ya Halmashauri
  • facebook ya Halmashauri
  • Matokeo ya Taifa Darasa la Saba 2016 Siha
  • kuomba pasipoti kupitia mtandaoni
  • WARAKA WA MAVAZI KWA WATUMISHI WA UMMA
  • Fomu za Likizo Watumishi wa Umma

Viunganisho Vinavyohusiana

  • Basic Education Statistics
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Takwimu za taifa
  • Idara ya habari maelezo
  • tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Wananchi Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotazama

free HitCounter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji,Halmashauri ya Wilaya ya Siha /Siha District Council

    sanduku la Posta: 5 BR- Sanya Juu -Elerai S.L.P 129, 25482 SIHA

    simu: 0272-970677

    Mobile: 0713164432 DED Siha

    Email: ded@sihadc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani Ya eneo

Copyright ©2017 SihaDistrictCouncil . All rights reserved.