• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Serikali |
    • Malalamiko |
Siha District Council
Siha District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serekali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Siha

  • Mwanzo
  • Historia
    • Dhima na Dira
    • Wasifu wa Wilaya
  • Utawala
    • Muundo wa Kiutawala
    • Idara
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Kilimo,Ushirika na Umwagiliaji
      • Idara ya Mipango,Takwimu na Umwagiliaji
      • Idara ya Elimu Msingi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
    • Kata
      • Sanya Juu
      • Gararagua
      • Karansi
      • Biriri
      • Songu
      • Makiwaru
      • Olkolili
      • Ormelili
      • DonyoMuruak
      • Ngarenairobi
      • Ndumet
      • Mitimirefu
      • Livishi
      • Nasai
      • Kirua
      • Kashashi
      • Ivaeny
  • Huduma zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za maji
    • huduma za Watumishi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Tourism
  • Machapisho
    • Fomu za Maombi
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria
    • Jarida Mtandaoni Kila mwezi
  • Kituo cha habari
    • Maktaba ya Picha
    • Videos
    • Hutuba
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Elimu,Afya na Maji
      • Ujenzi,Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
      • Wajumbe Mkutano wa ALAT
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba vikao 2022/2023
    • Ratiba M/Kiti Halmashauri

Baraza la Ardhi na Nyumba lafunguliwa rasmi Wilaya ya Siha

Posted on: August 17th, 2023

MKUU WA MKOA  AFUNGUA BARAZA LA ARDHI NA NYUMBA  WILAYA YA  SIHA

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu amefungua Baraza la ardhi na nyumba  Wilaya ya Siha na kuwaapisha wajumbe wa baraza hilo.

Mhe. Babu amesema hayo agosti 16, 2023 katika hafla ya kuwaapisha wajumbe wanne na kuzindua baraza la ardhi na nyumba Wilaya ya Siha iliyofanyika katika ofisi ya mkuu wa Wilaya ya siha na kuongeza kuwa mabaraza ya ardhi ya kata na wilaya hayana viashiria vitakavyowafanya wananchi kuogopa/kuwa na hofu ya kupeleka mashauri ya ardhi na nyumba kwa ajili ya usuluhishi.

Amesema mkoa wa Kilimanjaro umebarikiwa kuwa na ardhi nzuri  yenye rutuba hivyo wananchi wanatakiwa kuitumia ardhi hiyo kwa ajili ya uzalishaji na kujiongezea kipato badala ya kugombana kila wakati kutokana na migogoro ya ardhi,ameongeza kuwa  uwepo wa mabaraza ya ardhi na nyumba yatasaidia kupunguza na kuondoa migogoro ya ardhi katika  Wilaya ya Siha na Mkoa wa Kilimanjaro kwa ujumla.

Naye mkuu wa Wilaya ya Siha Mhe. Dkt Christopher Timbuka amesema kuzinduliwa kwa baraza la ardhi na nyumba Wilaya ya Siha kutawarahisishia wananchi kupunguza  gharama ya ukupeleka kesi zao Mkoani  kwani awali walikuwa wakitumia gharama kubwa kufuata huduma hiyo Makao Makuu ya Mkoa yaliyopo Moshi hali iliyokuwa ikisababisha kushindwa kupata haki kutokana na gharama kuwa kubwa.

Amesema kufunguliwa kwa baraza hilo kutawasaidia viongozi wa Wilaya kufanya kazi nyingine za kuwaletea maendeleo wananchi wa Wilaya ya Siha badala ya kukaa maofisini kutatua kesi na migogoro ya ardhi.

“Wapo baadhi ya Wananchi walipoteza haki yao baada ya kushindwa kusafiri kwenda Moshi kutokana na gharama za kwenda hadi huko na ilikuwa kilio kikubwa katika Wilaya yetu ya Siha, Hivyo ujio wa baraza hili utaturahisishia sana kazi katika Wilaya ili sisi tufanye kazi nyingine ya kuwaletea wananchi maendeleo ” Alisema Dkt. Timbuka.

Kwa upande wake, msajili wa msaidizi wa mabaraza ya ardhi na nyumba  kanda ya Kaskazini Zena Mathias amewataka wajumbe wa baraza la ardhi Wilaya ya Siha walioapishwa na mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu kuwa waadilifu na kutendea haki viapo vyao kwa kuwahudumia vema  wananchi wa Wilaya ya Siha.

Pia amewaomba wajumbe walioapishwa kujitoa kwenye mashauri yenye mgongano wa kimaslahi yanayowasilishwa katika baraza hilo ili kufanya kazi kwa weledi na kwa ufanisi kwa kufuata sheria na kanuni zinazowaongoza katika kutimiza majukumu yao.

“Wajumbe ambao mmeapishwa na Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro mjue kwamba hii ni dhamana mmepewa kwa ajili ya kuwahudumia wananchi wa Wilaya ya Siha, kwa hiyo naomba sana  mtumie vizuri  dhamana mliyopewa  msije mkawaangusha wananchi wanaowategemea kupata haki katika mashauri watakayoleta katika baraza” Alisema Zena.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA WALIOITWA KAZINI SIHA DC OKTOBA 2024 October 21, 2024
  • TANGAZO LA KOSEGEZWA MBELE UKODISHAJI WA MASHAMBA January 22, 2025
  • TANGAZO NAFASI YA MWENYEKITI BODI YA AJIRA HALMASHAURI YA SIHA KILIMANJARO February 18, 2025
  • TANGAZO NAFASI ZA KAZI SIHA August 28, 2020
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • Rais Samia aendelea kuitangaza Tanzania Kimataifa

    April 11, 2025
  • Rais Samia aendelea kuitangaza Tanzania Kimataifa

    April 11, 2025
  • Uzinduzi Sera ya Ardhi Siha yashiriki

    March 17, 2025
  • Umoja wa Ulaya kuendelea kushirikiana na Tanzania

    March 12, 2025
  • Ona Zote

Video

WATUMISHI SIHA DC WAASWA KUFANYA KAZI KWA UADILIFU
Video zingine

Viunganisho vya haraka

  • Wasifu wa Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Wasifu wa Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri
  • Soma taarifa zote ndani ya tovuti
  • Blog ya Halmashauri
  • facebook ya Halmashauri
  • Matokeo ya Taifa Darasa la Saba 2016 Siha
  • kuomba pasipoti kupitia mtandaoni
  • WARAKA WA MAVAZI KWA WATUMISHI WA UMMA
  • Fomu za Likizo Watumishi wa Umma

Viunganisho Vinavyohusiana

  • Basic Education Statistics
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Takwimu za taifa
  • Idara ya habari maelezo
  • tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Wananchi Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotazama

free HitCounter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji,Halmashauri ya Wilaya ya Siha /Siha District Council

    sanduku la Posta: 5 BR- Sanya Juu -Elerai S.L.P 129, 25482 SIHA

    simu: 0272-970677

    Mobile: 0713164432 DED Siha

    Email: ded@sihadc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani Ya eneo

Copyright ©2017 SihaDistrictCouncil . All rights reserved.